Watu wengi wamekuwa wakijiuliza maswali mbalimbali ambayo yanahusiana na masuala ya kibiashara. Na miongoni mwa maswali ambayo wamekuwa wakiniuliza ni kuhusu ni nini faida ya kutangaza biashara kwa sehemu kubwa?
Swali hili ndilo limenifanya nishike kalamu yangu ili niweze kulijibu. Nakusihi twende sambamba ili niweze kueleza kwa kinagaubaga, kwa nini unapaswa kuitangaza biashara yako tena kwa nguvu zote.
Matangazo ni usambazaji wa taarifa sahihi kuhusu bidhaa au huduma kutoka kwa mfanyabiashara kwenda kwa mteja. Matangazo ndiyo roho ya biashara, kwani bila kufanya biashara yako bila matangazo ni sawa na bure.
Nafikiri pia utakubaliana nami ya kuwa ili uweze kufanya biashara yenye tija ni lazima uitangaze biashara yako, kwani " biashara ni matangazo". Matangazo ndiyo yatakuyokufanya uweze kuongeza mauzo ya kibiashara kila wakati.
Kwa kuzingatia hilo unaweza kuitangaza biashara yako kwa njia ambayo itakuwa ni rahisi kwako. Na sababu kubwa ya kuitangaza biashara yako ni kuongeza wateja wapya.
Leo na dhumuni kubwa la kutangaza biashara yako ni kukutana na na watu wapya, ukiona umetangaza biashara yako na hakuna mteja mpya hata mmoja ujue fika kuna mahala ambapo umekosea.
Hivyo fanya tathimni upya na ujipange upya na kuona ni jinsi gani unaweza kuitangaza biashara hiyo. Vile vile katika upangaji wa malengo ya kibiashara hakikisha ya kwamba unapanga na mbinu za kukutana na watu wapya kila siku.
Nasisitiza juu ya kukutana na watu wapya, kwa sababu nimegundua ya biashara nyingi zimekuwa hazifanyi vizuri kwa sababu zimekuwa na watu ambao wanaizunguka biashara ile ni wale wale kila siku. Hivyo kila siku fanya tathimini juu wateja wapya ambao wamekuja katika biashara yako.
Asante kwa kutembelea mtandao huu wa dira ya mafanikio, usisite kumshirikisha na mwingine ili aweze kujifunza.
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025 Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025, NBC Premier League Tanzania Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Na Mbuke Shilagi Kagera. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mradi wa umeme wa maji ya maporomoko wa Rusumo...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imetupilia mbali shauri lililokuwa limefunguliwa na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina...