Monday, May 17, 2021

Felix Kavejuru atangazwa mshindi wa ubunge jimbo la Buhigwe


Felix Kavejuru (CCM) ametangazwa mshindi katika uchaguzi mdogo wa ubunge  jimbo la  Buhigwe uliofanyika jana Jumapili Mei 16, 2021.

Akitangaza matokeo usiku wa kuamkia leo Jumatatu Mei 17, 2021 msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, Marrycelina Mbehoma amesema Kavejuru amepata  kura 25,274 akifuatiwa na mgombea wa  ACT-Wazalendo,   Garula Tanditse aliyepata  kura 4,749.

Amebainisha wapiga kura walioandikishwa ni 112,333 lakini waliojitokeza kupiga kura ni 30,713. Amesema  kura halali zilikuwa 30,320 na zilizoharibika 593.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...