Sunday, May 9, 2021

Breaking : SERIKALI YATANGAZA NAFASI ZA AJIRA...UALIMU, AFYA... KUOMBA MWISHO MEI 23

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu, ametangaza nafasi za ajira kwa walimu 6,949 wa shule za Msingi na Sekondari pamoja na ajira 2,726 kwa kada mbalimbali za Afya.

Amesema ajira hizo ni utekelezaji wa agizo lililotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, la kuajiri wafanyakazi zaidi ya elfu sita.

Akizungumza Jijini Dodoma leo Mhe.Ummy amesema ajira hizo zinakwenda kuziba mapengo ya wafanyakazi waliostaafu, waliofariki na wengine kuacha kazi hivyo ajira hizo ni za watanzania na kwa wale watakaokidhi vigezo watapatiwa ajira kwa haraka ili kutoa huduma bora kwa wananchi.

Ameongeza kuwa ajira zitatolewa kwa haki na waombaji wasitoe fedha yeyote ili kupata ajira kwakuwa baadhi ya watu wanaweza kutumia vibaya fursa hiyo.

Watu wenye sifa wanatakiwa kuomba kuanzia leo Mei 9 hadi 23, 2021.

*********

Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR -TAMISEMI) imepata kibali cha ajira za Watumishi wa Kada mbalimbali za Afya 2,726 kwa ajili ya Hospitali za Halmashauri, Vituo vya Afya na Zahanati pamoja na Walimu 6,949 wa Shule za Msingi na Sekondari watakaofanya kazi chini ya Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini.

Kwa sababu hiyo, wahitimu kutoka kwenye Vyuo vya Elimu ya Juu, Vyuo vya Ualimu na Vyuo vya Afya vinavyotambuliwa na Serikali wanatangaziwa kutuma maombi yao ya nafasi za kazi kuanzia tarehe 09-23 Mei, 2021.

Nafasi za ajira zilizopo ni kwa wahitimu wa Astashahada (Certificate), Stashahada (Diploma) na Shahada (Degree). 

A: TARATIBU ZA KUOMBA AJIRA ZA UALIMU

Walimu wote wenye sifa watume maombi kwa njia ya mtandao kupitia kiunganishi cha ajira.tamisemi.go.tz kwa utaratibu ufuatao:

-i.Walimu wote wenye sifa ambao hawakuomba ajira za ualimu (tarehe 07.09.2021) watume maombi yao kwa njia ya mtandao kupitia kiunganishi cha ajira.tamisemi.go.tz;

ii.Walimu walioomba ajira kwa njia ya mtandao kufuatia Tangazo la Ajira la tarehe 07 Septemba, 2020, wanaelekezwa kuingia kwenye akaunti zao walizotumia wakati wa kutuma maombi ili kuhakiki usahihi wa taarifa na viambatisho walivyotuma hapo awali; na

iii.Tangazo hili linawahusu wahitimu wa Kozi za Ualimu kuanzia mwaka 2012 hadi mwaka 2019.

2.0 SIFA ZA WAOMBAJI

2.1SIFA ZA KITAALUMA ZA MWOMBA JI

Walimu wanaotakiwa kutuma maombi wawe na Sifa za kitaaluma kama ifuatavyo:

2.1.1 WALIMU WA SHULE ZA MSINGI

Walimu wanaoomba kuajiriwa kufundisha Shule za Msingi wawe na Sifa zifuatazo:

i.Mwalimu Daraja la III

A: Mhitimu wa Astashahada ya Ualimu Elimu ya Msingi, Astashahada ya Ualimu Elimu ya Michezo, Astashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Astashahada ya Ualimu wa Elimu Maalum;

ii.Mwalimu Daraja la III

B:Mhitimu wa Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Awali, Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Msingi na Stashahada ya Ualimu wa Elimu Maalum;na iii.Mwalimu Daraja la III

C:Mhitimu wa Shahada ya Ualimu katika masomo ya "English Language, History na Geography".

2.1.2 WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI

i.Mwalimu Daraja la III

B:Mhitimu wa Stashahada ya Ualimu wa Masomo ya "Physics, Mathematics, Biology na Chemistry";ii.Mwalimu Daraja la IIIC:Mhitimu wa Shahada ya Ualimu aliyesomea Elimu Maalum kwa Masomoya "Physics, Chemistry, Biology naMathematics";

iii.Mwalimu Daraja la IIIC:Mhitimu wa Shahada ya Ualimu wa Masomo ya "Physics, Mathematics, Chemistry na Biology"; naiv.Mwalimu Daraja la IIIC:Mhitimu wa Stashahada ya Uzamili katika Elimu (Post Graduate Diploma in Education) lazima awe mwenye Shahada ya Kwanza (Bachelor Degree) yenye Masomo yaliyotajwa katika (ii) na iii) hapo juu.

2.2. WAHITIMU WALIOSOMA NJE YA NCHI

i.Waombaji wote waliosoma Elimu ya Sekondari nje ya nchi wanatakiwa kupata Namba ya Ulinganifu wa Matokeo (Equivalent Number) inayoanza na Herufi EQ...kutoka Baraza la Mitihani la Tanzania ili kuwawezesha kuingia kwenye Mfumo wa Ajira; na

ii.Waombaji waliosoma Vyuo Nje ya Nchi wanatakiwa kupata Ithibati ya masomo yao kutoka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ili vyeti vyao viweze kutambuliwa na kupata uhalali wa kutumika hapa nchini.

3.0 SIFA ZA JUMLA ZA MWOMBAJI WA AJIRA ZA UALIMU

Mwombaji wa nafasi zilizoainishwa hapo juu awe na sifa za jumla zifuatazo:

-i.Awe ni Mtanzania;

ii.Awe na umri usiozidi miaka arobaini na tano (45);

iii.Awe hajawahi kufukuzwa, kuacha kazi au kustaafishwa katika Utumishi wa Umma;

iv.Awe na namba ya kitambulisho cha Taifa;

v.Waombaji wenye Shahada na Stashahada za NACTE na TCU (UDOM) waambatishe Cheti cha Kuhitimu Mafunzo na "Transcript".

Waombaji wa Astashahada na Stashahada za NECTA waambatishe Cheti cha Mafunzo katika sehemu mbili (weka cheti na weka "transcript");

vi.Nakala ya Cheti cha Kidato cha Nnena Sita; vii.Nakala ya Cheti cha Kuzaliwa;naviii.Maelezo Binafsi (CV), yakionesha umri, anuani kamili na namba ya simu ya kiganjani.

B:TARATIBU ZA KUOMBA AJIRA KADA ZA AFYA

Wataalamu wa Kada za Afya wenye sifa watume maombi kwa njia ya mtandao kupitia kiunganishi cha ajira.tamisemi.go.tz: -2.0

Sifa za Waombaji ni kama ifuatavyo:-

2.1DAKTARI DARAJA LA II

Waombaji wawe na Shahada ya Udaktari wa Binadamu kutoka Vyuo Vikuu/Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali waliomaliza Mafunzo ya Kazi "Internship" ya muda usiopungua mwaka mmoja na kupata Usajili kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika).

2.2 DAKTARI WA MENO DARAJA LA II

Waombaji wawe na Shahada ya Udaktari wa Binadamu kutoka Vyuo Vikuu/Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali waliomaliza Mafunzo ya Kazi "Internship" ya muda usiopungua mwaka mmoja na kupata Usajili kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika).

2.3 TABIBU DARAJA LA II

Waombaji wawe na Stashahada ya Utabibu (Diploma in Clinical Medicine) ya muda wa miaka mitatu kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

2.4 TABIBU MSAIDIZI

Waombaji wawe wamehitimu Astashahada ya miaka miwili ya Tabibu Wasaidizi (Clinical Assistants Certificate) kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

2.5 TABIBU WA MENO DARAJA LA II Waombaji wawe na Stashahada ya Tabibu Meno (Diploma in Clinical Dentistry) ya muda wa miaka mitatu kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

5.6TABIBU MENO MSAIDIZI

Waombaji wawe wamehitimu Astashahada ya miaka miwili ya Tabibu Wasaidizi (Clinical Assistants Certificate) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.

2.7 MFAMASIA DARAJA LA II

Waombaji wawe na Shahada ya Famasi kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali waliohitimu Mafunzo kwa Vitendo (Internship) ya mwaka mmoja na ambao wamesajiliwa na Baraza la Famasi (Pharmacy Council).

2.8 MTEKNOLOJIA (DAWA) DARAJA II

Waombaji wawe na Stashahada katika fani ya Uteknolojia wa Dawa (Diploma in Pharmaceutical Technology) kwa muda wa miaka mitatu kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwa na Baraza la Famasi (Pharmacy Council).

2.9 MTEKNOLOJIA MSAIDIZI (DAWA)

Waombaji wawe na Astashahada katika fani ya Uteknolojia wa Dawa ya Afya (Certificate in Pharmaceutical Technology) kwa muda wa miaka miwili kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwa na Baraza la Famasi (Pharmacy Council).

2.10 MTEKNOLOJIA (MAABARA) DARAJA II

Waombaji wawe na Stashahada katika fani ya Uteknolojia wa Maabara ya Afya (Diploma in Health Laboratory Sciences) kwa muda wa miaka mitatu kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwa na Baraza la Wataalamu wa Maabara za Afya (Health Laboratory Practitioners' Council).

2.11MTEKNOLOJIA MSAIDIZI (MAABARA)

Waombaji wawe na Astashahada katika fani ya Uteknolojia wa Maabara ya Afya (Certificate in Health Laboratory Sciences) kwa muda wa miaka miwili kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwa na Baraza la Wataalamu wa Maabara za Afya (Health Laboratory Practitioners' Council).


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...