Monday, April 5, 2021

RAIS SAMIA ATENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI ALIYEMTEUA JANA USIKU


Rais Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Thobias Mwesiga ambaye aliteuliwa jana, kufuatia uamizi huo Rais Samia amemrejesha Dkt.James Mataragio kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TPDC.

Dkt. Mataragio ndiye alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa TPDC kabla ya uteuzi wa Mwesiga kutangazwa hapo jana April 04,2021, Mataragio anaendelea na majukumu yake mara moja.



Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...