Mkuu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akitoa taarifa kuhusu kazi kubwa iliyofanyika katika mkoa wa Shinyanga kutokomeza ndoa na mimba za utotoni pamoja na kupinga ukatili wa kijinsia.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Shirika la Msichana Initiative kwa kushirikiana na UN Women wakiongozana na Machampioni wao wa kutokomeza ndoa za utotoni wakiwemo wabunge na viongozi mbalimbali wamefanya ziara mkoani Shinyanga na kufanya kikao cha pamoja na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack, Sekretarieti ya mkoa, Kamati ya ulinzi wa mwanamke na mtoto, kamati ya amani ya mkoa na wadau wa ndoa za utotoni mkoa wa Shinyanga ili kujadili namna ya kushirikiana pamoja kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Kikao hicho kimefanyika leo Jumamosi Aprili 10,2021 kikiwa na lengo kujadili mafanikio na mikakati ya kupambana na matukio ya ndoa za utotoni kimefanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Msichana Initiative, Rebeca Gyumi amesema wamekuja kujifunza mikakati inayofanyika mkoani Shinyanga katika kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto zikiwemo ndoa za utotoni ili kuangalia namna ya kutumia mikakati hiyo katika maeneo mengine nchini.
"Tumekutana na wadau wa ndoa za utotoni mkoani Shinyanga ikiwa ni sehemu ya ziara ya Shirika la Msichana Initiative tukiongozana na Machampioni wetu wa kutokomeza ndoa za utotoni ambao ni wabunge na baadhi ya viongozi mbalimbali",amesema Rebeca.
"Kupitia ziara hii tukaona ni muhimu Machampioni wakae kwenye kikao pamoja na mkuu wa mkoa wa Shinyanga,sekretarieti ya mkoa wa Shinyanga,kamati ya ulinzi wa mwanamke na mtoto,kamati ya amani ya mkoa na wadau wa ndoa za utotoni mkoa wa Shinyanga ili kujua jitihada zinazofanywa mkoani Shinyanga katika mapambano dhidi ya ndoa za utotoni na nini tufanye kwa pamoja kama njia ya kuhakikisha hili suala linatokomezwa",ameeleza Rebeca.
Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini, Aida Khenani ambaye ni miongoni mwa Machampioni hao amesema suala la ukatili dhidi ya wanawake na watoto siyo jambo la Shinyanga tu bali ni la nchi nzima hivyo wamekuja kuchukua mbinu zilizotumika mkoani Shinyanga katika kulinda mtoto wa kike akieleza kuwa wamepata uzoefu mpya wa jinsi ya kukabiliana na changamoto ya ukatili kwa mtoto wa kike.
"Kazi mliyoifanya Shinyanga ni kubwa sana. Niwapongeze sana kwa kuandaa kuunda Mpango Mkakati wa Mkoa wa Miaka mitano wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto 2020-2025, naona mmeandika kwa lugha ya Kiingereza naomba muandike pia kwa lugha ya Kiswahili ili hata wananchi wa kawaida waweze kuelewa na kuachana na vitendo vya ukatili",amesema Khenani.
"Ili kutokomeza ukatili Sheria peke yake haiwezi kumaliza tatizo hili ambalo lipo nchi nzima. Lakini pia ni lazima tumshirikishe mwanaume kwa sababu ndiyo chanzo. Ni lazima pia wadau wote tushirikiane, tuachane na mila na desturi zinazomkandamiza mtoto wa kike",ameongeza.
Akitoa taarifa kuhusu kazi kubwa iliyofanyika katika mkoa wa Shinyanga kutokomeza ndoa na mimba za utotoni pamoja na kupinga ukatili wa kijinsia, Mkuu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amesema mkoa wa Shinyanga umefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kupambana na ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na kumaliza mauaji ya watu wenye ualbino na vikongwe kufuatia mikakati kabambe iliyowekwa na mkoa huo.
Telack amesema miongoni mwa mikakati iliyofanyika ni kufanya utafiti na kuwabaini na kuwakamata watu waliokuwa wanawakata mapanga watu wenye ualbino na vikongwe.
"Baada ya Mhe.Rais kutupa dhamana ya kumsaidia kazi katika mkoa wa Shinyanga mwaka 2016,tulianza kwa kubaini changamoto kubwa zilizokuwepo katika mkoa wetu wa Shinyanga ambapo changamoto kubwa ilikuwa ni mauaji ya watu wenye ualbino,vikongwe na ukatili wa kijinsia unaojumuisha kuwapa mimba mabinti wadogo,ubakaji,mila na desturi kandamizi kwa wanawake",amesema Telack.
Amesema kufuatia takwimu za utafiti wa Maendeleo ya watu na afya Tanzania (TDHS,2010) zilizoonesha kwamba mkoa wa Shinyanga ulikuwa unaongoza kwa kuwa na ndoa za utotoni kwa asilimia 59, kitendo hicho hakikumfurahisha akaamua kuwaita viongozi wenzake na wadau mbalimbali na kuweka mikakati thabiti ya kukomesha changamoto hizo zote.
"Tulijipa muda wa kufanya utafiti wa kuwabaini wale wote waliokuwa wanawakata mapanga watu wenye ualbino na vikongwe. Tulifanya utafiti huu kwa siri kubwa, tuliwatumia wananchi wenyewe katika ngazi za vijiji wakati wa kupata taarifa,tuligundua kwamba wakata mapanga wakifanya uhalifu huo walikuwa wanakimbilia mikoa ya jirani kwa hiyo tukashirikiana na viongozi wenzetu wa mikoa jirani",ameeleza Telack.
"Baada ya utafiti wetu wa siri kukamilika,tulianza kuwakamata mmoja baada ya mwingine mpaka tukawamaliza wote.Baada ya kujiridhisha kwamba wote wamekamatwa,tukawafikisha kwenye vyombo vya sheria na tukaendelea kuzisimamia kesi hizo mpaka haki ikatendeka. Tangu mwaka 2016 hadi mauaji ya watu wenye ualbino na vikongwe katika mkoa wetu imebaki historia na sasa ukisikia kuna mauaji basi ni yale yanatokana na ugomvi wa mashamba watoto wakitaka kurithi ardhi ambayo nayo tunaendelea na mikakati ya kuhakikisha nayo yanakoma",ameongeza Telack.
Amesema pia waliunda na kutoa mafunzo ya kamati za ulinzi na usalama wa wanawake na watoto kuanzia ngazi ya mkoa hadi kijiji na mpaka sasa kuna kamati moja ya mkoa, kila halmashauri na kata 130 kila kata ina kamati moja na kamati zote zimepewa mafunzo ya Mpango Kazi wa Taifa wa Kudhibiti Ukatili dhidi ya wanawake na Watoto.
Amefafanua kuwa mkoa huo umeendelea kufanya vikao mbalimbali na taasisi mtambuka za serikali zinazohusiana na kesi za watoto na akina mama wanaofanyiwa ukatili ili kuwa na nguvu ya pamoja na kuharakisha upelelezi wa makosa yote ya jinai yanayohusiana na ukatili wa kijinsia pamoja na mimba na ndoa za utotoni.
"Pia tumetoa mafunzo kwa wasaidizi 223 wa huduma za msaada wa kisheria juu ya haki ya ustawi wa watoto pamoja na kukutana na waganga wa kienyeji,viongozi wa kimila na viongozi wa dini ili kuondoa mila na desturi kandamizi kwa wanawake na watoto",ameeleza.
"Tuligundua kuwa wananchi wengi wanaojihusisha na vitendo viovu kwa wanawake na watoto hawana hofu ya Mungu hivyo tukaamua kuunda Kamati ya Amani ya Mkoa yenye wajumbe 10 kutoka madhehebu mbambali ya dini,tukaipa jukumu la kuwafikia wananchi wote ndani ya mkoa na kuzungumza nao kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia na sasa wananchi wameanza kubadilika kwa kuingiwa na hofu ya Mungu",amesema Telack.
Ameongeza kuwa ili kuondoa kabisa changamoto ya ukatili wa kijinsia pamoja na na kutokomeza mimba na ndoa za utotoni,mkoa wa Shinyanga uliamua kuunda Mpango Mkakati wa Mkoa wa Miaka mitano wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto 2020-2025 (Five years Shinyanga Regional Strategic Plan to End Violence Against Women and Children – RSP-VWC,2025).
Mkuu huyo wa mkoa amesema kufuatia mikakati hiyo kabambe,hivi sasa kesi zote zinazohusisha ukatili wa aina yoyote ile kwa mtoto wa kike zinafanyiwa kazi haraka kwa kukamilisha uchunguzi pamoja na mahakimu kutoka hukumu kwa wakati.
Aidha amempongeza Mkurugenzi wa Taasisi ya Msichana Initiatives, Rebeca Gyumi kwa kazi kubwa anayoifanya katika kusimamia haki za mtoto wa kike.
Mkuu huyo wa mkoa ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wazazi kuzungumza na watoto wao kuhusu masuala ya ukatili na kuhakikisha wazazi wote (baba na mama) wanashiriki katika malezi ya watoto badala ya watoto kulelewa na mama pekee ama dada wa nyumbani.
Pia ameeleza kuwa mkoa wa Shinyanga una mpango wa kuleta mabasi kwa ajili ya kuwapeleka wanafunzi shuleni ambapo wazazi watakuwa wanawapa nauli watoto wao.
Akiwasilisha maazimio ya kikao hicho, Mratibu wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto kutoka Shirika la Women Fund Tanzania (WFT) mkoa wa Shinyanga, Glory Mbia amesema wamekubaliana kuzuia uzururaji wa mtoto,kuanzisha mabasi ya kubeba watoto na kuzuia watoto kwenda kuchunga mifugo pamoja na kuhakukisha marekebisho ya sheria ya ndoa 1971 yanafanyika bungeni na kualika mkoa wa Shinyanga na wadau waende bungeni kutoa uzoefu kuhusu Mpango Mkakati wa Mkoa wa Miaka mitano wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto 2020-2025.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akitoa taarifa kuhusu kazi kubwa iliyofanyika katika mkoa wa Shinyanga kutokomeza ndoa na mimba za utotoni pamoja na kupinga ukatili wa kijinsia kwenye kikao cha wadau wa kutokomeza ndoa za utotoni kilichoandaliwa na Shirika la Msichana Initiative kwa kushirikiana na UN Women wakati wa ziara ya Machampioni wa kutokomeza ndoa za utotoni mkoani Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akizungumza wakati akitoa taarifa kuhusu kazi kubwa iliyofanyika katika mkoa wa Shinyanga kutokomeza ndoa na mimba za utotoni pamoja na kupinga ukatili wa kijinsia kwenye kikao cha wadau wa kutokomeza ndoa za utotoni kilichoandaliwa na Shirika la Msichana Initiative kwa kushirikiana na UN Women wakati wa ziara ya Machampioni wa kutokomeza ndoa za utotoni mkoani Shinyanga.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Msichana Initiative, Rebeca Gyumi akizungumza kwenye kikao cha wadau wa kutokomeza ndoa za utotoni kilichoandaliwa na Shirika la Msichana Initiative kwa kushirikiana na UN Women wakati wa ziara ya Machampioni wa kutokomeza ndoa za utotoni mkoani Shinyanga
Mkurugenzi wa Taasisi ya Msichana Initiative, Rebeca Gyumi akizungumza kwenye kikao cha wadau wa kutokomeza ndoa za utotoni kilichoandaliwa na Shirika la Msichana Initiative kwa kushirikiana na UN Women wakati wa ziara ya Machampioni wa kutokomeza ndoa za utotoni mkoani Shinyanga
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa mtoto na mwanamke Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye kikao. Mbele kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP, Debora Magiligimba akifuatiwa na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga ACP Elizabeth Mbezi (katikati) na Mwakilishi wa Afisa Uhamiaji mkoa wa Shinyanga (Mwanasheria wa Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga) Elizabeth Godfrey Kaka wakiwa kwenye kikao cha wadau wa kutokomeza ndoa za utotoni kilichoandaliwa na Shirika la Msichana Initiative kwa kushirikiana na UN Women wakati wa ziara ya Machampioni wa kutokomeza ndoa za utotoni mkoani Shinyanga
Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini Mhe. Aida Khenani na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza Mhe. Ng'wasi Damas Kamani (kulia) ambapo ni Ma Champion wa kutokomeza ndoa za utotoni wakiwa kwenye kikao cha wadau wa kutokomeza ndoa za utotoni kilichoandaliwa na Shirika la Msichana Initiative kwa kushirikiana na UN Women wakati wa ziara ya Machampioni wa kutokomeza ndoa za utotoni mkoani Shinyanga
Wanaharakati wa haki za wanawake (Champion wa kutokomeza ndoa za utotoni) John Myola na Nancy Sumari wakiwa kwenye kikao cha wadau wa kutokomeza ndoa za utotoni kilichoandaliwa na Shirika la Msichana Initiative kwa kushirikiana na UN Women wakati wa ziara ya Machampioni wa kutokomeza ndoa za utotoni mkoani Shinyanga
Mwenyekiti Jumuiya ya Wanawake wa Kiislamu Tanzania (JUWAKITA) Hajat Shamim Khan ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Amani taifa akionesha Mpango Mkakati wa Mkoa wa Shinyanga Miaka mitano wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto 2020-2025 (Five years Shinyanga Regional Strategic Plan to End Violence Against Women and Children – RSP-VWC,2025) ambapo ameupongeza mkoa wa Shinyanga kwa kuandaa mpango huo na kushauri waandaaji wa mpango huo wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack waitwe bungeni kuelezea ili mikoa mingine iige ili kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya wanawake na watoto.
Kikao kinaendelea
Mwenyekiti Jumuiya ya Wanawake wa Kiislamu Tanzania (JUWAKITA) Hajat Shamim Khan ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Amani taifa akizungumza kwenye kikao cha wadau wa kutokomeza ndoa za utotoni kilichoandaliwa na Shirika la Msichana Initiative kwa kushirikiana na UN Women wakati wa ziara ya Machampioni wa kutokomeza ndoa za utotoni mkoani Shinyanga
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza Mhe. Ng'wasi Damas Kamani akizungumza kwenye kikao cha wadau wa kutokomeza ndoa za utotoni kilichoandaliwa na Shirika la Msichana Initiative kwa kushirikiana na UN Women wakati wa ziara ya Machampioni wa kutokomeza ndoa za utotoni mkoani Shinyanga ambapo alisema ili kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ni lazima wanaume pia washirikishwe katika mapambano hayo.
Mjumbe wa Kamati ya Amani Mkoa wa Shinyanga Sheikh Balilusa Khamis akizungumza kwenye kikao cha wadau wa kutokomeza ndoa za utotoni kilichoandaliwa na Shirika la Msichana Initiative kwa kushirikiana na UN Women wakati wa ziara ya Machampioni wa kutokomeza ndoa za utotoni mkoani Shinyanga ambapo alisema kamati hiyo inaunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali na wadau katika kulinda haki za wanawake na watoto.
Katibu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa wanawake na watoto Mkoa wa Shinyanga Tedson Ngwale akizungumza kwenye kikao cha wadau wa kutokomeza ndoa za utotoni kilichoandaliwa na Shirika la Msichana Initiative kwa kushirikiana na UN Women wakati wa ziara ya Machampioni wa kutokomeza ndoa za utotoni mkoani Shinyanga
Mkurugenzi wa shirika la Investing in Children and their Societies(ICS), Kudely Sokoine akizungumza kwenye kikao cha wadau wa kutokomeza ndoa za utotoni kilichoandaliwa na Shirika la Msichana Initiative kwa kushirikiana na UN Women wakati wa ziara ya Machampioni wa kutokomeza ndoa za utotoni mkoani Shinyanga
Mratibu wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto kutoka Shirika la Women Fund Tanzania (WFT) mkoa wa Shinyanga, Glory Mbia akizungumza kwenye kikao cha wadau wa kutokomeza ndoa za utotoni kilichoandaliwa na Shirika la Msichana Initiative kwa kushirikiana na UN Women wakati wa ziara ya Machampioni wa kutokomeza ndoa za utotoni mkoani Shinyanga
Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini Mhe. Aida Khenani akizungumza kwenye kikao cha wadau wa kutokomeza ndoa za utotoni kilichoandaliwa na Shirika la Msichana Initiative kwa kushirikiana na UN Women wakati wa ziara ya Machampioni wa kutokomeza ndoa za utotoni mkoani Shinyanga
Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini Mhe. Aida Khenani akiomba Mpango Mkakati wa Mkoa wa Shinyanga Miaka mitano wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto 2020-2025 (Five years Shinyanga Regional Strategic Plan to End Violence Against Women and Children – RSP-VWC,2025) uandikwe pia kwa lugha ya Kiswahili
Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga, Beda Chamatata akizungumza kwenye kikao cha wadau wa kutokomeza ndoa za utotoni kilichoandaliwa na Shirika la Msichana Initiative kwa kushirikiana na UN Women wakati wa ziara ya Machampioni wa kutokomeza ndoa za utotoni mkoani Shinyanga
Wadau wakiwa kwenye kikao cha wadau wa kutokomeza ndoa za utotoni kilichoandaliwa na Shirika la Msichana Initiative kwa kushirikiana na UN Women wakati wa ziara ya Machampioni wa kutokomeza ndoa za utotoni mkoani Shinyanga
Wadau wakiwa kwenye kikao cha wadau wa kutokomeza ndoa za utotoni kilichoandaliwa na Shirika la Msichana Initiative kwa kushirikiana na UN Women wakati wa ziara ya Machampioni wa kutokomeza ndoa za utotoni mkoani Shinyanga
Wadau wakiwa kwenye kikao cha wadau wa kutokomeza ndoa za utotoni kilichoandaliwa na Shirika la Msichana Initiative kwa kushirikiana na UN Women wakati wa ziara ya Machampioni wa kutokomeza ndoa za utotoni mkoani Shinyanga
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa mtoto na mwanamke Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye kikao. Mbele kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP, Debora Magiligimba na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga ACP Elizabeth Mbezi (kulia) wakiwa kwenye kikao cha wadau wa kutokomeza ndoa za utotoni kilichoandaliwa na Shirika la Msichana Initiative kwa kushirikiana na UN Women wakati wa ziara ya Machampioni wa kutokomeza ndoa za utotoni mkoani Shinyanga
Wadau wakiwa ukumbini
Kikao kinaendelea
Kikao kinaendelea
Kikao kinaendelea
Kikao kinaendelea
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack, meza kuu wakipiga picha ya kumbukumbu na Ma Champion wa Kutokomeza ndoa za utotoni
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack, meza kuu wakipiga picha ya kumbukumbu na Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa watoto na wanawake mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack, meza kuu wakipiga picha ya kumbukumbu na Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa watoto na wanawake mkoa wa Shinyanga na Sekretarieti ya mkoa
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack, meza kuu wakipiga picha ya kumbukumbu na Wadau wa haki za wanawake na watoto kutoka mashirika mbalimbali.
Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog