Monday, April 12, 2021

Mwanamfalme Harry atahudhuria vipi mazishi ya Babu yake?




Mtawala wa Sussex, Mwanamfalme Harry atarejea Uingereza kwa mara ya kwanza wiki hii kuhudhuria mazishi ya Babu yake katika Kanisa la Mtakatifu George ndani ya Kasri la Windsor.
Mwanamfalme Harry pamoja na mkewe Meghan Markle walijitoa kushiriki majukumu ya kifalme mwezi Machi Mwaka jana.

Kama ilivyo kwa wasafiri wengine kutoka nje ya Uingereza, atatakiwa kufuata masharti yote ya serikali kuhusu tahadhari juu ya janga la virusi vya corona.

Mazishi ya Babu yake, ambaye ni mume wa Malkia, Mwanamfalme Philip yatafanyika siku ya Jumamosi.

Haopana. TMwanamfalme Harry ataungana na Familia ya Kifalme akitokea Marekani ambako anaishi na familia yake bila ya mkewe.

Kwa mujibu wa Kasri la Buckingham, Bi Meghan, ambaye ni mjamzito ameshauriwa na daktari wake asisafiri.

Kukaa karantini kwa siku 10 na kufanya vipimo vya Covid-19 siku ya pili na ya nane baada ya kuwasili Uingereza.

Hata hivyo kuna ruhusa ya kuacha baadhi ya kanuni kutokana na hali fulani. Mathalani hautatakiwa kukaa Karantini kama unaingi Uingereza kutoka eneo linalohesabika kaama ni moja katika safari za anga, mathalani nchi ya Ireland.

Karantini ya siku 10 kwa Mwanamfalme Harry haitakuwa katika hoteli (kwa kuwa Marekani haipo katika orodho ya nchi ambazo Uingereza imeziweka katika mstari mwekundu wa hatari ya maambukizo).

Ushauri wa serikali ni kuwa wasafiri kutoka nchi hizo wanaweza kukaa karantini majumbani mwao, "wakiwa na marafiki na famialia" ama katika hoteli au makazi ya muda.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...