Wednesday, April 7, 2021

Konde Boy Afunguka Mashabiki Kumuita Messi





KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Luis Miquissoine 'Konde Boy' raia wa Msumbiji ameibuka na kuweka wazi juu ya mashabiki wa timu hiyo kumfananisha na mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi.

 

Luis ametoa kauli hiyo ikiwa amefanikiwa kuifungia mabao matatu katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi akiwa mchezaji pekee wa timu hiyo aliyetupia zaidi mpaka sasa akifuatiwa na Mzambia, Claotus Chama mwenye mawili.



Staa huyo mwenye kasi uwanjani amefichua kuwa mmoja sababu ya mashabiki kumuita Messi imetokana na yeye kujituma zaidi ndani ya uwanja hivyo anachukulia sawa kwa kuwa inampa nguvu ya kuendelea kupambana.

 

"Unajua watu kwenye soka wanapenda kufananisha chochote kile ambacho wao wanaona kitakuwa kinafaa zaidi kwao mimi ni Miquissoine nitabakia kuwa hivyo kwa sababu nacheza aina ya mpira wangu ambo nimeuzoea.

 

"Lakini watu wengi wamezoea kunifananisha hata kama wao wananiambia kwamba mimi ni Messi naona sawa kwa sababu Messi ni mchezaji mkubwa ila najivunia kwa kuwa ananipa nguvu zaidi ya kuweza kupambana na kufunga zaidi," alisema Miquissone

STORI: IBRAHIM MUSSA, Dar es Salaam


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...