Wednesday, April 14, 2021

Jimbo la New Mexico lahalalisha bangi kwa matumizi ya starehe


Gavana wa jimbo la New Mexico Michelle Lujan Grisham Jumatatu alitia saini, muswada wa bangi uliopitishwa na bunge la jimbo hilo mwezi uliopita, na kufanya jimbo hilo kuwa la 17 kuidhinisha mihadarati hiyo kwa ajili ya matumizi ya starehe.

Lujan Grisham alichochea kupitishwa kwa sheria ya bangi mwezi uliopita, na kuweka sahihi yake ni katika kufuata tu taratibu.

Alisema ''sheria hii ni hatua, hatua kubwa kwa jimbo letu,'' aliandika katika ukurasa wake wa twitter.

''Kuhalalisha matumizi ya bangi kutabadilisha namna tunavyofikiri kwa mustakabali mzuri wa New Mexico, nguvu kazi yetu, uchumi wetu, kesho yetu.

Wakati bunge la jimbo la New Mexico likipiga kura kuhalalisha bangi mwishoni mwa mwezi uliopita, walikuwa wakifanya hivyo saa kadhaa baada ya Gavana Andrew Cuomo kuweka saini kuhalalisha muswada wa bunge la jimbo la New York uliopitishwa usiku uliotangulia.

Kuhalalishwa kwa matumizi ya bangi kwa watu wazima kulikopitishwa na majimbo hayo mawili katika kipindi cha saa 24 kunaonesha namna gani hatua hii inavyoendelea kukua kwa kasi.

"Huu ni ushindi muhimu kwa New Mexico," Lujan Grisham aliandika wakati huo, akitoa mfano wa upatikanaji wa ajira mpya na mapato mapya ya ushuru.

'Bangi ilikuwa ikichomwa wakati wa ibada' na Waisraeli wa zamani - utafiti unasema

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...