Sunday, April 11, 2021

Idadi waandamanaji waliouwawa Myanmar yapindukia 700

 


Mlinzi mmoja amejuruhiwa na mripuko wa bomu leo hii katika benki inayomilikiwa na jeshi mjini, Mandalay, katika kipindi ambacho pia idadi ya vifo vilivyotokana na ukandamizaji wa jeshi vikiongozeka na kupindukia zaidi ya watu 700.


Benki ya Myawaddy, tawi kubwa kabisa mjini Mandalay, ambalo lililengwa Asubuhi ya leo, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya taifa hilo mlinzi wake amejeruhiwa na mripuko huo. Kulionekana idadi kubwa ya maafisa wa usalama kufuatia mkasa huo.


Benki hiyo ni moja kati ya biashara zinazodhibitiwa na jeshi ambazo zimekabiliwa na shinikizo la kususiwa tangu kutokea mapinduzi, na wateja wengi wanadai kutoa fedha zao.


Kumekuwa na matukio ya umwagikaji damu zaidi katika siku za hivi karibuni ambapo jana Jumamosi, waangalizi nchini humo walisema vikosi vya usalama vimewauwa waandamanaji 82 katika tukio lilitokea Ijumaa, katika mji wa Bago, uliopo umbali wa kilometa 65 kaskazini/mashariki mwa Yangon.


Myanmar imeingia katika mkwamo mwezi Feburuari Mosi baada ya jeshi limuondoe madarakani mtawala wa kiraia, Aung San Suu Kyi.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...