Na Thabit Madai, Zanzibar.
MKURUGENZI mtendaji wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC) Harusi Miraji Mpatani amewataka asasi za kiraia Nchini kuwa na mitazamo yakinifu wakati wa utatuzi wa migogoro katika Jamii.
Pia aliwataka wana Asasi hizo za Kiraia kufaya kazi kwa kuzingatia weledi na utu ili wasiwe chanjo cha mgogoro.
Wito huo ameutoa wakati akiwasilisha mada katika mafunzo maalumu ya kuwajengea uwezo Asasi za kiraia Zanzibar juu ya namna ya kutatua migogoro mbalimbali katika jamii ambapo mafunzo hayo yamefanyika katika ukummbi wa ZLSC uliopo kijangwani Mjini Unguja.
Mkurugenzi huyo alieleza kwamba, katika jamii kila mmoja huwa na mitazamo yao kulingana na mambo wanavyoyaona hivyo Asasi za kiraia wanatakiwa kuwa na mitazamo yakinifu ambayo itasaidia kwa kiasi kikubwa wakati wa utatuzi wa migogoro katika jamii.
"Tunapokwenda kutatua migogoro katika jaminii jambo la msingi ni kusikiliza watu kwanza, kasha kutoa maamuzi yaliyoyakinifu kutokana nay ale tuliyoyasikiliza," alisema.
Aliwaeleza kwamba hawatakiwi kutoa maamuzi bila ya kuwasiliza na kuchukulia jambo kwa upana wake ili kila upande uridhike na maamuzi yaliyotolewa.
tunatakiwa kusikiliza watu, na kulichulia jambo kwa upana wake ili maamuzi tukitoa kusiwe na upande mmoja ambao hautaridhia," alisema.
Hata hivyo aliwataka wana Asasi za kiraia kuhakikisha wanafanya kazi kwa kuzingatia weledi wa kazi pamoja na utu ili wasiwe chanjo cha kuleta migogoro badala ya kutatua.
"Kazi kubwa ya Asasi za kiraia kuhakikisha wanatatua migogoro na si kuchangia kuleta migogoro katika jamii, hivyo munatakiwa kuhakikisha kwamba munafanya kwa kuzingatia weledi na utu katika majukumu yenu ya kila siku," alisema.
"Kikubwa munapoihudumia jamii jambo la muhimu sana kufanya kazi kwa kuzingatia utu ili jamiii iweze kuwaamini na musiwe chanjo cha migogoro,"alifafanua.
Katika hatua nyingine Mpatani aliwaeleza kwamba wanatakiwa kuhakikish Amani na utulivu ya nchi iliyopo inaendelea kutunzwa.
"Katika majukumu yenu hakikisheni kwamba Amani na utulivu wan chi munaendelea kuitunza kwa namna yoyote,"alieleza.
Nae Afisa ufuatiliaji na Tathimini wa mradi huo aliwaeleza washiririki wa mafunzo hayo kuhakikisha wanasikiliza vyema mafunzo hayo na kwenda kuyatumia katika majukumu ya ya kila siku.
Mafunzo hayo yameandaliwa na kituo cha huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC) chini ya ufadhili wa Umoja wa ulaya (European Union ) katika kutekeleza mradi wa 'JENGA AMANI YETU' ambao unahusisha maenep mbalimbali Tanzania bara na visiwani.