Majaji nchini Marekani wamemkuta na hatia ya mauaji Derek Chauvin, polisi mzungu wa zamani wa Minneapolis kufuatia kifo cha Mmarekani mweusi George Floyd, katika kesi ambayo iliyoonekana kama mtihani kwa uwajibikaji wa polisi nchini Marekani.
Majaji walijadiliana chini ya saa 11 kabla ya kumtia hatiani Chauvin katika mashtaka yote matatu ya mauaji dhidi yake.Chauvin mwenye umri wa miaka 45 alipatikana na makosa ya mauaji ya kiwango cha pili, kiwango cha tatu na mauaji bila kukusudia.
Umati mkubwa wa watu ulliokuwa umekusanyika nje ya mahakama ya Minneapolis walifurahia kwa shangwe uamuzi huo, huku wengine wakitokwa na machozi baada ya wiki tatu za kuiskiliza kesi hiyo.
Chauvin anakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 40 jela kwa shtaka la kwanza, ambalo ni mauaji ya bila kukusudia. Hukumu itatolewa siku nyengine.