Saturday, February 20, 2021

Waziri Akar azungumzia Mkutano wa NATO


Waziri wa Ulinzi wa Kitaifa Hulusi Akar amezungumzia kuhusu Mkutano wa Mawaziri wa Ulinzi wa NATO na kusema,

"Tulisisitiza umuhimu wa washirika wanaofanya kazi kwa umoja na mshikamano katika vita dhidi ya ugaidi."

Mkutano huo wa Mawaziri wa Ulinzi wa NATO ulifanyika siku 2 kwa njia ya video ambapo Waziri Akar aliwakilisha Uturuki na kutoa maelezo yafuatayo,

"Tumewajulisha washirika wetu wazi kwamba vizuizi vya idhini, majaribio na vitisho dhidi ya nchi yetu vinadhoofisha muungano."

Akibainisha uhitaji wa nguvu moja kwa washirika wote ili kuhakikisha uimara wa muungano, Akar aliongezea kusema,

"Tulisisitiza umuhimu wa washirika wanaofanya kazi kwa umoja na mshikamano katika vita dhidi ya ugaidi."

"Uturuki, ambayo inaadhimisha miaka 69 ya ushirika wa NATO, itaendelea kutimiza ahadi zake kwa ukamilifu na kuchukua jukumu kubwa kwa ajili ya muungano." 


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...