Monday, February 8, 2021
Taarifa Ya Utekelezaji Maamuzi Ya Serikali Kuhusu Migogoro Ya Matumizi Ya Ardhi Katika Vijiji 975 Yawasilishwa
Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvu amewaoongoza Mawaziri wenzake wa Wizara za Kisekta kupokea taarifa ya utekelezaji wa maamuzi ya Serikali kuhusu Migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 vilivyopo katika hifadhi na Mapori ya Akiba.
Taarifa hiyo iliwasilishwa na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mary Makondo tarehe 4 Februari 2021 jijini Dodoma kwa niaba ya Kamati ya Mawaziri na Wataalamu kutoka Wizara za Kisekta.
Wizara za kisekta zinazoshiriki ni Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Maliasili na Utalii, Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ofisi ya Makamu wa Raisi, Wizara ya Ulinzi na Wizara ya Maji. Aidha, katika kikao hicho Wizara za Mambo ya Ndani Nchi, Wizara ya Katiba na Sheria na Wizara ya Fedha zilialikwa kutokana na umuhimu wa wizara hizo katika utekelezaji wa maamuzi.
Akizungumza wakati wa uwasilishwaji taarifa hiyo, Waziri wa Ardhi William Lukuvi alisema, mbali na mambo mengine Taarifa ya vijiji 975 vyenye migogoro ya matumizi ya ardhi itawezesha Mawaziri wa Wizara husika aliowaeleza kuwa, wengi wao ni wageni kujua mpango mkakati na namna ya utekelezaji wa maamuzi ya Serikali kuhusiana na kunusuru vijiji 975.
''Hapa wengi wenu ni wageni karibu asilimia 80, hivyo taarifa inayowasilishwa leo itawasaidia kujua utekelezaji wa maamuzi ya serikali kuhusiana na migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975'' alisema Lukuvi.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mary Makondo alisema kupitia kikao hicho kuwa, pamoja na Kamati kutekeleza maamuzi ya Serikali kuhusiana na migogoro ya matumizi ya ardhi kwenye vijiji 975, wizara yake imetekeleza pia baadhi ya mambo kwa lengo la kupunguza migogoro ya matumizi ya ardhi kama vile kuandaa mpango wa matumizi ya ardhi katika vijiji 114 vinavyozunguka hifadhi.
Utekelezaji wa maamuzi ya Serikali kuhusiana na migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 nchini unafuatia kukithiri kwa migogoro ya ardhi ambapo, Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Februari 2019 aliunda Kamati ya Mawaziri wa Kisekta chini ya Waziri wa Ardhi William Lukuvi ili kutafuta ufumbuzi wa kudumu.
Kufuatia mapendekezo ya Kamati, Baraza la Mawaziri mnamo mwezi Septemba, 2019, liliridhia kuwa vijiji 920 kati ya vijiji 975 vilivyokuwemo ndani ya hifadhi na mapori visiondolewe.
Source
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Na Mbuke Shilagi Kagera. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mradi wa umeme wa maji ya maporomoko wa Rusumo...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025 Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025, NBC Premier League Tanzania Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Msanii wa nyimbo za asili Nyanda Madirisha Obhado 'Maliganya' maarufu Shikomba Bhulolo anakualika kusikiliza wimbo wake mpya 2021 un...
-
Ninakualika kutazama Video Mpya kabisa mwaka 2021 kutoka kwa Msanii Yobat amemshirikisha Bhudagala Ng'wana Malonja na Shija Kadoke wim...
