Tuesday, February 9, 2021

Serikali yatenga mabilioni kununua vifaa vya hospitali

 


Serikali ya Tanzania imetenga Sh33.5 bilioni kwa ajili ya kununua vifaa tiba kwa ajili ya hospitali 67 za halmashauri nchini.


Hayo yamesemwa leo Jumanne Februari 9, 2021 na naibu waziri wa Tamisemi,  Dk Festo Ndugange leo Jumanne Februari 9, 2021 wakati akijibu swali la mbunge wa Mbogwe (CCM),  Nicodemus Maganga.


Maganga katika swali lake la nyongeza amehoji ni lini Serikali itapeleka vifaa vya upimaji ikiwemo X- ray na vingine katika hospitali ya wilaya ya Mbogwe.


Akijibu swali hilo Dk Ndugange amesema Serikali imetenga Sh33.5 bilioni kwa ajili ya hospitali 67 za  halmashauri ambapo Mbogwe ni miongoni mwa hospitali hizo.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...