Wednesday, February 24, 2021

Nategemea kulivunja Jiji la DSM, tunaweza kuifanya Ilala kuwa Jiji- JPM


 "Nategemea kulivunja Jiji la DSM, tunaweza kuifanya Ilala kuwa Jiji lakini kuwa na Madiwani wanakaa hapa juu, hawana miradi ya maendeleo wanakula posho na hawakuchaguliwa na Watu hili nitalikataza, Manispaa moja DSM ipandishwe hadhi kuwa Jiji na nyingine zibaki kuwa Manispaa" Rais MAGUFULI Akiwa Ubungo Jijini Dar Es Salaam

"Wale wanaojiandaa kuwa Mameya wa Jiji la DSM na hawana maeneo wajue hicho kimekwisha, tunataka manispaa moja ya Jiji la DSM ndio ipandishwe hadhi iwe Jiji halafu nyingine ziwe Manispaa, kama kwenye Majiji mengine, mjiandae kisaikolojia waliokuwa wanataka Umeya wa DSM" Rais MAGUFULI Akiwa Ubungo Jijini Dar Es Salaam

"Jiji la Dar es salaam litaendelea kuwepo lakini tutachukua eneo fulani na nafikiri Ilala inafaa kuwa Jiji kwa sababu ndio katikati ya Mji, Ubungo itasubiri kidogo kwa kuwa hata Barabara bado hazijatengenezwa, lazima tuijenge DSM ya kisasa, liwe Jiji kweli la kisasa" Rais MAGUFULI Akiwa Ubungo Jijini Dar Es Salaam


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...