Thursday, February 4, 2021

MBUNGE NEEMA AITAKA SERIKALI ITATHIMINI KAMA TOZO ZINAZOPUNGUZWA ZITAMNUFAISHA MKULIMA MDOGO

 

MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) kupitia NGOs Neema Lugangira

MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) kupitia NGOs Neema Lugangira amesema hatua ya Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Magufuli kwa kufuta tozo 168 zilizohusu Kilimo,Mifugo na Uvuvi na Biashara itasaidia kuimarisha uwekezaji na kunufaisha wakulima wadogo nchini.

Neema aliyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma wakati alipopata nafasi ya kuchangia katika Hoja ya Hotuba ya Mhe Rais Dkt John Magufuli ambapo katika hotuba yake kwenye ukarasa wa 25 alisema katika miaka mitano iliyopita alifuta tozo 168 .

Alisema kati ya hizo 114 zilihusu kilimo,mifugo na uvuvi na 54 za biashara na wataendelea na hatua hizo mwisho wa kumnukuu ambapo alisema jambo hilo litasaidia kuimarisha uwekezaji na kunufaisha wakulima wadogo kupitia mapato,

Mbunge Neema alisifu jitihada ambazo zinafanywa na Serikali ya awamu ya tano kwa kufanikisha hilo huku akiishauri serikali  kufanya tathimini ili kuweza kujiridhisha punguzo za tozo hizo kama pia zinawanufaisha wakulima wadogo kama wanavyotarajia.

Aidha aliiomba Serikali iagize wadau wote kufanya tathimini ya tozo zote zilizotolewa maana kwa uzoefu wake unaonyesha kwamba wakati mwengine tozo hizo hazina matokeo ya haraka kufika kwa wakulima wadogo ipasavyo.

"Nikushukuru sana Mh Spika kwa kunipa nafasi hii ili nami pia niweze kuchangia hotuba ya Mhe Rais napenda kujielekeza kwenye sekta ya kilimo na hivyo naamini uimarishaji wa mazingira ya ufanyaji biashara unatakiwa uende sambamba na unufaikaji wa wananchi"Alisema

Alisema jambo la pili katika Hotuba ya Mhe Rais ambalo angependa kuchangia ni katika hotuba yake kwenye ukurasa wa 26 ambapo amesema kwamba kwa msingi huu kwenye kilimo wanakusudi kuongeza tija na kufanya kiweze kuwa cha biashara lengo ni kujihakikishia usalama wa chakula.

"Lakini pia Mhe Rais alielekeza upatikanaji wa malighafi za viwandani na pia kupata ziada ya kuuza nje ili kufanikisha hayo ntutahakikisha zana bora za kilomo ikiwemo mbegu,viwatilifu ,mbolea,uukuaji dawa na matrekta vinapatikana kwa beii nafuu"

Mbunge huyo aliendelea kuipongeza serikali kwa kazi kubwa waliyoifanya kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita na hotuba ya Rais imesisitiza yale yaliyoandikwa kwenye ilani ya CCM katika kifungu 35 hadi 46 hivyo ili tuweze kufanikisha hayo kwa kasi angependa kushauri yafuatayo.

Alisema cha kwanza ni lazima wajikite kwenye uzalishaji wa aina mbalimbali za mbegu maana hivi sasa ukienda kwenye duka la mbegu utakuta asilimia 80 zimetoka nje ya nchi.

Ambapo katika hilo aliishauri serikali kuzijengea uwezo taasisi za ndani na binafsi za ithibati (local certification bodies) kwani kufanya hivyo tutaweza kufanikisha mbegu tunazozalisha hapa nchini nazo ziweze kuuzwa nje ya nchi.

Hata hivyo alisema kwamba amekubaliana na mapendezo yaliyopo kwenye ilani ya CCM kuhusu Wizara ya kilimo kuwa na bodi ya mazao na taasisi ambazo zinahitaji kupitiwa upya kimuundo ili ikiwezekana kuwa na taasisi chache zitakazoongeza ufanisi na usimamizi wa sekta hiyo.

Alisema hivyo kwa sababu wingi wa hizo bodi za mazao na taasisi unaleta mkanganyiko mkubwa kwenye sekta hivyo unakinzana na dhana nzima ya kuimarisha mazingira wezeshi ya uwekzaji na biashara kwa ujumla,

Mbunge Neema alitoa wito kwa wadau wa sekta ya kilimo kuwa mstari wa mbele kuhamaisha uzalishaji na ulaji wa vyakula nyenye viini lishe vingi ili kuungana na juhudi za serikali kutokomeza udumavu na utapiamlo kwa ujumla.

"Kama tunavyofahamu Tanzania asilimi 32 ya watoto chini ya miaka 5 wamedumaa kwa hiyo kila watoto 100 watoto 32 wamedumaa na inashangaza kwamba mikoa inayoonza kwa hali hiyo inaongozwa kwa uzalishaji wa chakula" Alisema Mbunge huyo.

Hata hivyo alitoa wito kwa wadau hao pamoja na kuhamasisha uzalishaji wa mazao ya kibiashara badala yake wahamasishe ulaji wa mazao yenye viini lishe vingi ambayo ipo kwenye Ilani  CCM
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...