Tuesday, February 23, 2021
Dkt . Chaula : Juhudi Za Pamoja Zinahitajika Katika Mazingira Ya Kukuza Matumizi Bora Ya Mawasiliano Nchini.
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma
Katibu mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt.Zainabu Chaula amesema juhudi za pamoja zinahitajika kutengeneza , mazingira ya kukuza matumizi bora ya mawasiliano nchini.
Dkt.Chaula amesema hayo leo Februari 23,2021 jijini Dodoma katika Kikao cha kujadili Mkakati wa TEHAMA kwenye ngazi ya jamii ikiwemo vituo vya Afya na shule hapa nchini ,Tanzania Community Digitization [TCD] kilichokutanisha wadau mbalimbali wa Mawasiliano.
"Juhudi hizi za pamoja zitatusaidia katika kukuza sekta ya mawasiliano zikiwemo ni pamoja na mkongo wa Taifa wa ;hii ni katika kuhakikisha mawasiliano yanafika katika ngazi zote hadi vijijini"amesema.
Aidha,Dkt.Chaula amesema moja ya malengo ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ni kuhakikisha taasisi zote za umma zinapata huduma ya Mawasiliano kwa gharama nafuu, ifikapo mwaka 2025 wizara itajipima angalau kufikia asilimia 40% .
Hata hivyo,Dkt.Chaula amebainisha kuwa serikali ya awamu ya tano imejipanga ni kwa namna gani inahakikisha inafikisha huduma ya mawasiliano katika maeneo mbalimbali ambapo wizara imetoa mwelekeo katika kusambaza huduma ya mawasiliano.
"Ndio maana serikali ina sera ya TEHAMA ya mwaka 2000 na mwaka 2016 serikali ilipitia sera ili kwendana na mazingira na maendeleo ya Teknolojia ,lazima tutengeneze mazingira ya Evaluation .Mwezi uliopita umefanya nini na sasa unafanya nini,na tunatambua mchango wa sekta binafsi katika mawasiliano hivyo tumejipanga katika kuhakikisha sekta ya mawasiliano inasonga mbele"amesema.
Pia ,Dtk.Chaula amesema vyombo vya Habari vina mchango mkubwa katika kuhabarisha umma juu ya umuhimu wa mawasiliano katika kukuza uchumi wa nchi.
Kwa upande wake Mkuu wa mifumo ya Habari USA, Desden Wengaa amesema wataendelea kushirikiana na Wizara katika Nyanja mbalimbali za mawasiliano.
"Kwa nanma moja ama nyingine wote tunahusika na jambo hili ,tumejenga mifumo mikubwa TAMISEMI ,kupitia level za halmashauri mpaka level za vijiji ,ili mifumo ifanye kazi vizuri lazima internet connection"amesema.
Mkurugenzi wa TEHAMA Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mulembwa Munaku amesema pamekuwepo na changamoto ya wadau wengi kupeleka huduma ya mawasiliano katika sehemu moja na wengine kukosa huduma hiyo .
Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya kutoa majukwaa ya mtandao wa kujifunzia kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari[Shule Direct] Faraja Nyarandu amesema mradi huo umekuja kwa muda muafaka katika kukuza sekta ya mawasiliano nyanja za elimu huku mkuu wa idara ya mawasiliano ya uhandisi na elektroniki kutoka chuo kikuu cha Dodoma Dkt.Florence Rashidi akibainisha wamejipanga kushirikiana na serikali .
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Bongo Deco wauzai wa vifaa mbalimbali vya umeme kama TV, Subwoofer, Hometheator, Majiko madogo na makubwa ya Gesi, Friji, Generator nk leo w...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia)akimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii wa Jamhuri ya ...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Kuongezeka kwa ghasia za hivi majuzi kumesababisha idadi kubwa ya raia wa Lebanon kukimbia kutoka Beirut huku milipuko ikitikisa jiji hilo...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 15, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekagua ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo – Busisi) ...