Thursday, February 11, 2021

Alikiba airudisha akaunti yake ya YouTube, atoa tangazo hili




Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Alikiba amethibitisha kuwa akaunti yake ya YouTube ya Alikiba sasa ipo mikononi mwaka.



Kupitia ukurasa wake wa Instagram alikiba amewaambia amshabiki wake wawe tayari na wasubscribe akaunti hiyo kwa ajili ya kupokea muziki wake.

Ikumbukwe alikiba baada ya kuachana na aliyekuwa meneja wake wa zamani Sevan Mosha ilielezwa kuwa akaunti hiyo ipo chini ya Seven na takribani mwaka sasa hakuwa anaitumia akaunti hiyo kwa ajili ya kuweka ngoma zake na badala yake alikuwa akitumia akaunti ya Kings music ambayo pia ipo chini yake ila nyimbo zinazoweka katika akaunti hiyo ni pamoja na za wasanii wa lebo hiyo.

Akaunti hiyo tayari ina subscriber zaidi ya  laki saba na tayari ameanza kuweka maudhui.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...