Thursday, January 21, 2021

Tanzia: Mbunge wa Ccm Manyara Martha Umbura afariki dunia


Na John Walter-Babati

Taarifa zilizothibitishwa na Katibu wa chama cha Mapinduzi mjini Babati Feisal Dauda zinaeleza kuwa Mbunge wa viti maalum mkoa wa Manyara Martha Umbura amefariki dunia.

Taarifa hiyo ambayo katibu wa Ccm Mjini Babati ameipakia katika ukurasa wake binafsi wa Facebook, haijaeleza chanzo cha kifo chake.

Martha Umbura amekuwa Mbunge wa viti maalum mkoa wa Manyara zaidi ya miaka kumi ambapo hadi anafariki alikuwa Mbunge wa viti maalum katika mkoa huo.

Mungu ailaze roho ya marehem mahali pema peponi, Amina



Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...