Watu wasiopungua 100 wanahofiwa kupoteza maisha kwenye shambulizi la angani lililoendeshwa katika mkoa wa Mopti nchini Mali.
Shambulizi hilo lilitekelezwa wakati wa sherehe ya harusi kwenye kijiji kimoja ambapo mpaka sasa aliyehusika hajulikani.
Kulingana na taarifa ya kituo cha redio cha Studio Tamani nchini Mali, iliarifiwa kwamba shambulizi la angani lilitekelezwa katika kijiji cha Bounti siku ya Jumapili nyakati za usiku wa kuamkia siku ya Jumatatu .
Meya wa mkoa huo Adama Griaba, alisema kuwa mhusika wa shambulizi hilo hajulikani na kwamba idadi ya vifo inaweza kuwa kati ya watu 100 na 150.
Kulingana na mashuhuda wa tukio hilo, idadi kubwa ya watu waliohudhuria harusi kijijini walifariki baada ya shambulizi hilo.
Idadi ya majeruhi kwenye shambulizi pia haijulikani.