Kama wewe ni mtu unayependa kujifunza kutenegeneza vitu vya kijasiriamali basi makala hii ni maalumu sana kwako.
Mahitaji:
1. Vibanio vyenye urembo mbalimbali.
2. Sponji zenye urembo mbalimbali.
3. Brash kubwa/ndogo.
4. Meza kubwa yenye urefu wa mita moja mpaka mbili.
5. Sufuria.
6. Vitambaa vya mpira.
7. Misumari midogo.
8. Jiko.
Madawa:
1. Sodium hydrosulphate.
2. Caustic soda
3. Mshumaa.
Kazi zake:
1. Sodium hydrosulphate ni kuimarisha rangi isichuje, kama itachanganywa na caustic soda. Madawa haya huwa kazi yake ni moja lakini ikikosekana moja nyingine haifanyi kazi.
2. Kazi ya mshumaa ni kuweka urembo kwenye nguo au kwenye vitambaa kwa kutumia vibao au sponji zenye urembo wa tembo, twiga, matunda au aina yoyote ya urembo unayotaka mtengenezaji.
Jinsi ya kutengeneza.
Jinsi ya kugonga mishumaa
Chemsha mshumaa uchemke sawasawa kisha ipua upoekidogo.Andaa kitambaa cha cotton na kukitandika mezani,chovya kibao chenye picha kwenye mshumaa kisha gonga kwenye kitambaa na kuacha nafasi kidogo. Endelea kugonga picha hizo mpaka kitambaa kiishe.
Jinsi ya kuweka rangi
Chemsha maji ya moto yachemke sawa sawa kisha pima lita tano mpaka sita. Baada ya hapo pima caustic soda vijiko3 na sodium hydrosulphate vijiko vinne mpaka vitano. Changanya na maji ya moto ,weka rangi kijiko kimoja. Baada ya hapo pima maji lita kumi na tano na changanya na mchanganyiko wa madawa ili maji yawe vuguvugu.Tumbukiza vitambaa vya vinne vya mita tatu kwa wakati mmoja na kuvigeuzageuza viingie rangi kwa dakika kumi mpaka kumi na tano. Suuza kwa maji baridi na uanike kwenye kivuri ili mshumaa usiyeyuke.
Kuweka rangi ya pili
Katika kuweka rangi hii kinachofanyika ni kuongeza vipimo vya ranagi tu. Ongeza vipimo vya rangi viwili na zaidi ya mala ya kwanza, maji, mudani uleule.
Weka mshumaa sehemu ambayo haina mshumaa kwa kutumia urembo uleule. Pima rangi kwa kufuata hatua zilezile. Tumbukiza vitambaa vitatu, geuza kwa mda uleule kisha anika.
Jinsi ya ufua mshumaa
Chemsha maji yachemke vizuri, changanya na sabuni ya unga jikoni, tumbukiza kitambaa kimoja kimoja jikoni ili kutoa mshumaa, geuza kwa mti, suuza kwenye maji ya baridi yaliyochanganywa na maji.
Piga pasi tayari kwa kuuza.
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Na Mbuke Shilagi Kagera. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mradi wa umeme wa maji ya maporomoko wa Rusumo...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025 Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025, NBC Premier League Tanzania Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Msanii wa nyimbo za asili Nyanda Madirisha Obhado 'Maliganya' maarufu Shikomba Bhulolo anakualika kusikiliza wimbo wake mpya 2021 un...
-
Ninakualika kutazama Video Mpya kabisa mwaka 2021 kutoka kwa Msanii Yobat amemshirikisha Bhudagala Ng'wana Malonja na Shija Kadoke wim...
