Kutoonekana kwa bilionea wa China na muasisi wa kampuni ya Alibaba Jack Ma katika kipindi cha runinga cha BBC, kinachoangazia mashujaa wa biashara Afrika ni kutokana na ratiba yake kumbana.
Katika kufafanua hilo ,msemaji wa Alibaba alisema: "Kufuatia kutoonekana kwa Jack Ma katika kipindi cha mashindano cha BBC cha 'Africa Business Hero competition', Jack ameshindwa kushiriki kutokana na ratiba zake kumbana."
Kwa mujibu wa vyombo kadhaa vya habari , vinasema bwana Ma hajaonekana katika umma kwa kipindi cha miezi miwili , tangu alipotoa maelezo ambayo yalikuwa na mkanganyiko kuhusu mfumo wa kibenki wa China katika shughuli moja ya umma huko Shanghai mnamo Oktoba 24.
Awali, kitengo cha fedha kinachofanya malipo mtandaoni kinachohusishwa na Alibaba, kilifanyiwa ukaguzi na mamlaka.
Alibaba haiwezi kudhibitisha au kukataa kutoonekana kwa bwana Ma katika umma, na haiwezi kueleza alipo Jack Ma.
Awali bilionea huyo hakuonekana kwa umma kwa kipindi cha miezi miwili , alirudi baada ya mwezi na kuomba radhi kwa kitendo walichokifanya.
Watu wa usalama wa China wanasema haijawa wazi kama Jack Ma anapaswa kuhofiwa kupotea.
Mfanyakazi wa zamani wa Alibaba aliiambia BBC kuwa si kawaida yake kuwa kimya kiasi hicho wakati wa sherehe za mwaka mpya wa China.
Lakini awali matukio kama hayo ya kutoweka kwa watu maarufu kama mcheza filamu Fan Bingbing kunaonesha kuwa kunaweza kuchukua miezi kadhaa.
Alibaba anamiliki asilimia 3 ya soko la hisa za Hong Kong.