Saturday, November 14, 2020
Watalii Wa Ndani Zaidi Ya 80 Watembelea Hifadhi Ya Ngorongoro
Na Kassim Nyaki-NCAA
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imepokea zaidi ya watalii wa ndani 80 kutoka benki ya CRDB kwa ajili ya kutembelea vivutio mbalimbali vinavyopatikana katika hifadhi hiyo ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha utalii wa ndani (domestic tourism).
Safari ya watalii hao iliyoratibiwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwa kushirikiana Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imelenga kutoa hamasa kwa watanzania kutembelea vivutio mbalimbali vinavyopatikana nchini ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Serikali kutangaza vivutio hivyo ambavyo vimekuwa na mchango mkubwa katika kuongeza pato la Taifa.
Mkurugenzzi wa Masoko wa TTB Mindi Kasiga aliyeambatana na ujumbe huo amebainisha kuwa, ujio wa wageni hao ni muendelezo wa juhudi za Serikali kuhamasisha watanzania na wageni wa mataifa mbalimbali kutembelea vivutio vya utalii vilivyoko nchini ili kutoa hamasa kwa wananchi.
"Nchi yetu imebarikiwa kuwa na vivutio vingi na vya kipekee duniani, TTB kwa kushirikiana na NCAA tumeandaa programu hii ikiwa ni muendelezo wa kuunga mkono juhudi za Serikali kutangaza vivutio vyetu ndani na nje ya nchi na tunafurahi kuona kwamba muoamko wa Watanzania kutembelea vivutio vyetu umezidi kuimarika kila mwaka"), aliongeza Kasiga.
Kwa upande wake Kamishna msaidizi mwandamizi wa UhIfadhi (huduma za Utalii) wa NCAA Bw. Paul Fissoo ameipongeza TTB na CRDB kwa kuleta kundi la wafanyakazi zaidi ya 80 kutembelea hifadhi hiyo kwa wakatii mmoja na kusisitiza kuwa utaratibu huo ni mfano mzuri wa kuigwa kwa mashirika mengine ya Serikali na Sekta binafsi kuandaa safari za pamoja na watumishi wao ili kutembelea vivutio vya hifadhi hiyo kwa bei nafuu kabisa ya shilingi 11,800 pekee.
Eneo la Hifadhi ya ngorongro ni eneo lenye vivutio vya kipekee duniani ikiwemo Crater ya Ngorongoro yenye Wanyama wa aina mbalimbali zaidi ya 25000, utalii wa kiutamaduni, makumbusho yenye historia ya chimbuko ya binadamu wa kale zaidi duniani (Zamadam), nyayo za binadamu wa kale, pia ni eneo pekee ambapo unaweza kuwaona Wanyama wakubwa watano (Simba, faru, Chui, Tembo na Nyati) kwa wakati mmoja katika eneo moja.
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe asomewa mashtaka matatu ya uchochezi, yenye nia ya kuleta ch...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Zikiwa zimesalia siku chache tu Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu 'SHY PARK HOTEL' ifunguliwe Rasmi mwezi Agosti 202...
-
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amefunga rasmi mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa ya...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
