Friday, November 20, 2020

Wasiofanya usafi wa mazingira kubanwa na sheria ndogondogo za halmashauri


N aTimothy Itembe Mara.

Mkuu wa wilaya Tarime,Ing Mtemi Msafiri amesema kuwa wasiofanya usafi wa mzingira katika maeneo yao wataendelea kubanwa na sheria ndogo za halmashauri.

Akiongea ofisini kwa mkuu wa wilaya Tarime,Ing Mtemi Msafiri na waandishi wa habari Kaimu usafi na mazingira wa  halmashauri ya Tarime vijijini,Martha Mahule, alisema kuwa wale wote ambao wanakaidi taratibu za kufanya usafi wa mazingira katika maeneo yao wataendelea kubanwa na sheria ndogo za halmasahauri  ikiwemo kupigwa faini.

Mahule aliongeza kuwa kufanya usafi wa mazingira  ni moja ya chanzo cha kuepukana magonjwa ya mlipuko ambayo yanatokea mara kwa mara kutokana mazingira kuwa machagu ikiwemo kutiririsha maji machafu na kinyesi cha Binadamu.

"Niwaombe ndugu zangu wajenge tabia ya kufanya usafi katika mazingira wanayokaa wasitegemee kusukumana na viongozi wa serikali kwani kufanya hivyo watakuwa wameepuka mkono wa sheria ndogo inayowabana wasiofanya usafi wa mazingira ikiwemo kutozwa faini"alisema Mahule.

Mhule alitumia nafasi hiyo kusema kuwa halmashauri yake imejipanga kupitia viongozi wa vitongoji na vijiji huku ikiwashirikisha wananchi katika kufanya usafi wa mazingira ambapo aliongeza kusema kuwa  wale ambao wanakaidi wanapigwa faini kadri wanavyo kubaliana katika mikutano yao ambapo fedha hiyo inabaki maeneo husika ili kufanya shuguli za maendeleo.

Naye Mjaya Bwire ambaye ni Afisa Afya wa halmashauri ya Tarime vijijini alisema kuwa jamii inatakiwa kujenga tabia ya kuwa na vifaa vya kuhifadhia taka ili gari la serikali linapokuwa linapita iwe rahisi kukusanya na kupeleka panapo husika.

Bwire aliwataka wakazi wa Tarime kujenga tabia ya kutunza mazingira ikiwemo vyanzo vya maji.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...