Sunday, November 15, 2020

Raia wa Brazil wapiga kura kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa


Sao Paulo, Raia wa Brazil wanapiga kura leo katika uchaguzi wa serikali za mitaa ambao utakuwa kipimo cha uthabiti wa mwelekeo mpya wa taifa hilo chini ya rais anayegemea siasa za mrengo wa kulia Jair Bolsonaro.


Uchaguzi huo tayari uliahirishwa kwa muda wa wiki sita kutokana na janga la virusi vya corona ambalo limewauwa zaidi ya watu 165,000 nchini Brazil, na linatishia kupunguza idadi ya wapiga kura watakaojitokeza.


Mamlaka za nchi hiyo zimewataka wapigakura kwenda na kalamu binafsi, kuheshimu masharti ya kujitenga na kushafisha mikono kila wakati watakapokuwa kwenye vituo vya kupigia kura.


Huu ni uchaguzi wa kwanza tangu rais Bolsonaro, afisa wa zamani wa jeshi, aliposhinda kwa kishindo mwaka 2018 na kubadili siasa za taifa hilo lenye uchumi mkubwa Amerika ya Kusini.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...