Serikali ya Armenia imewafuta kazi Mawaziri wa Ulinzi, Hali za Dharura na Kazi kufuatia uamuzi ulitiwa saini na rais wa nchi.
Kwa mujibu wa uamuzi huo uliosainiwa na Rais Armen Sarkisyan, Waziri wa Ulinzi David Tonoyan aliondolewa na Vagarshak Harutyunyan akachukua nafasi yake.
Waziri wa Hali za Dharura Feliks Tsolakyan pamoja na Waziri wa Kazi Zaruyi Batoyan pia walifutwa kazi kufuatia uamuzi huo.
Baada ya Waziri Mkuu Nikol Pashinyan kutangaza kuwa Armenia imeshindwa na Azerbaijan kwenye mapambano ya eneo la uvamizi la Nagorno-Karabakh, maandamano yalianzishwa na kumtaka Pashinyan ajiuzulu.
