Saturday, October 10, 2020

Watu 9 wakamatwa Hong Kong kwa kuwatorosha wanaharakati


Polisi Hong Kong imewakamata watu tisa leo wanaotuhumiwa kuwasaidia waandamanaji 12 na wanaharakati ambao walikamatwa baharini wakati wakijaribu kukimbilia Taiwan mnamo mwezi Agosti. Watu hao tisa ni wanaume wanne na wanawake watano, wa kati ya miaka 27 hadi 72. 


Wengine waliwahi kukamatwa wakati wa wamaandamano ya mwaka jana ya kupinga mswada wa serikali ambao ungeruhushu washukiwa wa makosa ya jinai wa Hong Kong kuhukumiwa China bara. Watu hao tisa waliokamatwa wanashukiwa kuwasaidia waandamanaji pamoja na wanaharakati kwa kuwapa malazi na msaada wa kifedha, kuwapatia boti ambayo iliwatorosha, na kuwatengenezea mipango ya maisha wakifika huko Taiwan.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...