Thursday, October 22, 2020

Wanamgambo 19 wa Al-Shabaab waangamizwa kwenye operesheni iliyoendeshwa na jeshi la Somalia


Wanamgambo 19 wa kundi la kigaidi la Al-Shabaab wameripotiwa kuangamizwa kwenye operesheni iliyoendeshwa nchini Somalia.

Vikosi vya jeshi la Somalia vimetoa maelezo na kuarifu kuangamizwa kwa wanamgambo 19 wa kundi la kigaidi la Al-Shabaab kwenye operesheni iliyoendeshwa eneo la Dinsoor mkoani Bay.

Jenerali Odowa Yusuf Rage alizungumza na kituo cha redio cha jeshi la Somalia na kubainisha kuwa walifanikiwa kuharibu kambi moja waliyokuwa wamekusanyika wanamgambo wa kigaidi.

Jenerali Odowa pia alisema kuwa operesheni hiyo iliendeshwa katika eneo la umbali wa takriban kilomita 11 kutoka Dinosoor kufuatia taarifa ya upelelezi iliyopokewa.

Katika wiki za hivi karibuni, jeshi la Somalia limekuwa likiendesha operesheni dhidi ya Al-Shabaab. Operesheni zaidi zimeendeshwa katika maeneo ya kusini mwa nchi.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...