Tuesday, October 27, 2020

Mchunguzi wa UN asema Belarus lazima ikome kuwatesa watu wake


Mchunguzi wa Umoja wa Mataifa wa haki za binaadamu kuhusu Belarus Anais Marin ameitaka serikali ya nchi hiyo kukoma kuwakandamiza watu wake, akisema karibu watu 20,000 walikamatawa Agosti na Septemba na mamia wameripotiwa kupigwa, kutishwa, kuteswa au kunyanyaswa kizuizini. 

Marin amenukuu duru kutoka Wizara ya Mambo ya ndani na mashirika yasiyo ya kiserikali kwa takwimu hizo na kusema wafungwa wengi wamejikuta wakikabiliwa na mashitaka ya kiutawala au uhalifu, akitaja zaidi ya kesi 400 za uhalifu dhidi ya waandamanaji tangu uchaguzi uliopingwa wa Agosti 9. 

Ombi la afisa huyo wa Umoja wa Mataifa limesisitizwa katika taarifa iliyowasilishwa kwa kamati hiyo kutoka kwa nchi 52 za Ulaya na Umoja wa Ulaya. 

Pia zimetoa wito wa kusitishwa mashambulizi dhidi ya waandamanaji wa amani, unyanyasaji kwa wale walioko kwenye vuguvugu la kudai demokrasia, kuwatisha viongozi wa upinzani, wanahabari, watetezi wa haki za binaadamu na waandamanaji.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...