Na huko nchini Uhispania idadi ya maambukizi ya virusi vya corona imepindukia milioni moja - kwa mara ya kwanza barani Ulaya.
Kulingana na Wizara ya Afya ya Uhispania, maambukizi yaliyothibitishwa hadi sasa ni 1,005,295.Idadi ya maambukizo mapya kwa kila wakaazi 100,000 ndani ya siku saba ni 178.
Hali hiyo inaifanya Uhispani kuwa na idadi kubwa zaidi ya maambukizi barani Ulaya na ya sita ulimwenguni kote.
Nchi zinazoongoza duniani kwa maambukizi ya virusi hivyo ni Marekani, India, Brazil, Urusi na Argentina.