Marekani na Japan leo zimeanza luteka kubwa ya kijeshi kuzunguka Japan katika kile kinaonekana kuwa ni onesho la nguvu za kijeshi kwa China ambayo miaka ya karibuni imezidisha shughuli zake za kijeshi kwenye kanda hiyo.
Luteka hiyo iitwayo ´Keen Sword `ni kwanza kufanyika tangu Yoshihide Suga alipochukua nafasi ya waziri mkuu wa Japan mwezi uliopita akiahidi kukabilina na kitisho cha China inayodai kumiliki visiwa vya Japan kwenye bahari ya mashariki.
Kamanda wa ngazi ya juu wa jeshi la Japan Koji Yamazaki amesema hali ya usalama kuzunguka Japan imekuwa ngumu na luteka hiyo ni nafasi muhimu ya kuonesha uthabiti wa ushirika uliopo kati ya nchi hiyo na Marekani Mazoezi hayo ya angani, ardhini na majini hufanyika kila baada ya miaka mwili na mwaka huu yanahusisha idadi kubwa ya meli na ndege za kivita pamoja na wanajeshi 46,000 kutoka Marekani na Japan.