Akua Asabea na mmewe
Akua Asabea, mwanamke aliyepata umaarufu mitandaoni baada ya picha zake na video yake na mzee ambaye ni mumewe kusambaa hatimaye amezungumza.
Katika mahojiano na kituo cha Ghanian, Asabea alisema kuwa,licha ya mumewe kuwa mzee , Akwasi Gyan, bado alikuwa na nguvu za kumtosheleza.
Kulingana na Asabea, mumewe ambaye ana umri wa miaka 97 kila wakati anamridhisha na kumlisha mahaba tele tele.
Asabea na Gyan walienea kwenye mitandao ya kijamii baada ya picha za harusi yao kuibuka mtandaoni.
Picha na video zilionyesha bwana harusi aliyeonekana mzee na bi harusi mwenye umri mdogo wakifanya harusi ya jadi ambayo ilizozua hisia mseto.
Kufuatia picha zao zilizosambaa kwa kasi, maharusi hao walihojiwa na vituo vingi ikiwemo Kofi TV ambayo ilizungumza nao.
Asabea alieleza kwamba alikubali kuolewa na Agyaba kwa sababu ya mapenzi na utu wake.
Mwanamke huyo mwa miaka 35 alifichua kwamba Agyamba, ambalo ni jina la matani la mumewe anatumia dawa fulani za kiasili zinazompa afya nzuri na nguvu zaidi.
Alidokeza kuwa yeye na mumewe wamekuwa katika uhusiano wa mapenzi kwa takriban miaka 14.
Murkomen amuambia Uhuru Wapenzi hao wana watoto wanne ambapo kifungua mimba ana miaka 11 na mdogo miaka mitatu.
Via Tuko News