Monday, October 19, 2020

China yasema Marekani inajifanya mhanga katika ripoti za kuwazuia raia wake

 


Wizara ya mambo ya nje ya China inasema Marekani inajifanya muhanga kufuatia China kuionya Marekani kwamba huenda raia wake wakazuiliwa nchini humo kutokana na hatua ya Marekani kuwafungulia mashtaka wasomi wa China. 

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Zhao Lijan amesema vitendo vya Marekani vimeharibu vibaya sana nia za raia wa China. 

Jarida la Wall Street Journal Jumamosi liliripoti kuwa maafisa wa China waliionya serikali ya Marekani mara kadhaa kwamba huenda China ikawazuia Wamarekani nchini humo kwa kulipiza hatua ya wizara ya ulinzi ya Marekani kuwafungulia mashtaka wasomi wa kijeshi wa China. 

Utawala wa rais Trump umeendelea kuituhumu China kwa kutumia operesheni za kimtandao pamoja na udukuzi kuiibia Marekani ujuzi wake wa kiteknolojia kama mkakati wa kuiondoa Marekani kama nchi inayoongoza kwa utajiri na nguvu za kijeshi duniani.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...