Saturday, October 17, 2020
Bweni Sekondari Uchira Islamic Lateketea kwa Moto
Bweni la Shule ya Sekondari ya wasichana ya Uchira Islamic iliyoko wilaya ya Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro, limeteketea kwa moto jioni ya Oktoba 16, 2020, huku chanzo cha moto huo kikiwa bado hakijajulikana mpaka sasa na hakuna kifo wala madhara kwa mwanafunzi yeyote.
Inspekta Abraham Ntezidyo, kutoka Jeshi la Zimamoto Mkoa wa Kilimanjaro, amesema taarifa za moto huo walizipata jana jioni majira ya saa 12:00 na moto umeteketeza jumla ya vitanda 25 ambavyo walikuwa wakilalia wanafunzi 50.
"Athari kubwa ni kwenye vitu vya wanafunzi na vitanda, wanafunzi hawakuwepo bwenini, walikuwa wameenda msikitini kwa ajili ya swala ya jioni, mpaka sasa hivi tunaendelea na uchunguzi wa moto huo ili kubaini chanzo na moto ulipoanzia," amesema Inspekta Abraham.
Aidha ameongeza kuwa, "Hapa wanafunzi wako katika hali ya mshtuko, mikakati iliyopo tunakagua shule moja baada ya nyingine kwa kushirikiana na vyombo vingine.
"Hata hii iliyoungua tunavyozungumza imekaguliwa juzi tu hata wiki haijaisha, lakini bahati mbaya imeungua, vyanzo vya moto viko vingi, kuna umeme, hujuma, kuna vingine vinasababishwa kwa makusudi".
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Na Mbuke Shilagi Kagera. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mradi wa umeme wa maji ya maporomoko wa Rusumo...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025 Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025, NBC Premier League Tanzania Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Msanii wa nyimbo za asili Nyanda Madirisha Obhado 'Maliganya' maarufu Shikomba Bhulolo anakualika kusikiliza wimbo wake mpya 2021 un...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
