Friday, June 5, 2020

Mamia waandamana Hong Kong wakidai demokrasia


Mamia ya waandamanaji wa Hong Kong wameandamana leo wakitoa kauli za kuunga mkono demokrasia, siku moja baada ya maelfu ya watu kukaidi amri ya polisi ya kufanya kumbukumbu ya ukandamizaji uliofanywa na China katika uwanja wa Tiananmen mwaka 1989.

 Waandamanaji walishiriki maandamano hayo ya amani katika eneo kuu la kibiashara la mji huo na maandamano hayo yakaisha kwa amani baada ya saa moja.

Maadhimisho ya jana ya ukandamizaji uliofanywa na China dhidi ya wanafunzi wa Hong Kong waliofyatuliwa risasi na polisi katika uwanja wa Tiananmen yalikuwa muhimu mno ukizingatia kuwa serikali kuu ya China imeiridhia rasimu ya sheria za usalama kwa mji huo.

Ilikuwa mara ya kwanza jana katika kipindi cha miaka 31 ambapo rabsha zilitatiza kile ambacho kinastahili kuwa siku ya huzuni kwa Hong Kong.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...