Rais wa Marekani Donald Trump amewaagiza Magavana wa Majimbo Nchini humo kufungua nyumba zote za ibada na Ibada ziendelee huku akisisitiza Watu kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya corona.
Trump amesema nyumba za ibada ambazo ni pamoja na makanisa, masinagogi na misikiti ni maeneo yanayotoa huduma muhimu kwa jamii.
Aidha amesema ikiwa magavana hao hawatotimiza agizo lake, basi atachukua hatua mikononi mwake kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo
"Nyumba za Ibada zinawaleta Watu pamoja na kuwaunganisha, fungueni, mwenye swali anipigie ila hatofanikiwa"- Alisema Trump
Maagizo ya Trump yametafsriwa na wengi kama hali flani ya kukubaliana na Msimamo wa Rais wa Tanzania Dr John Pombe Joseph Magufuli ambaye alikataa kuwafungia watu ndani kisa Corona na akasisitiza watu Wamuombe Mungu huku wakiendelea kuchukua tahadhari .
Dr Magufuli amekuwa akikaririwa mara kadhaa akisema kuwafungia watu kunawapunguzia kinga zao na hata kupuliza dawa barabarani hakuondoi Virusi vya Corona na kwamba Corona ni ugonjwa ambao utachukua muda mrefu kuisha kama ilivyo UKIMWI na magonjwa mengine.
Msimamo huo wa Rais Magufuli uliungwa mkono na Shirika la Afya Duniani WHO ambalo hivi karibuni lilitoa waraka ukisema kupuliza Dawa barabarani au sehemu za wazi hakuondoi virusi vya Corona, kujifungia ndani kunapunguza Kinga na kwamba ugonjwa huu utachukua muda mrefu kuisha.