Ufaransa imeripoti vifo vipya 642 kutokana na virusi vya corona.
Ripoti hiyo imetolewa na maafisa wa afya nchini humo.
Kati ya vifo hivyo, 368 walikuwa wakitibiwa hospitalini, wakati 278 walikuwa kwenye nyumba za wauguzi. Tangu kusambaa kwa virusi vya corona, jumla ya watu waliopoteza maisha ni 19,323.
11,842 walipoteza maisha wakiwa hospitalini na 7,481 katika nyumba za wauguzi.
Idadi ya wagonjwa waliolazwa imeshuka kutoka 31,190 hadi 30,639,wagonjwa 551 wamepungua.
Wagonjwa katika vyumba mahututi pia wamepungua kutoka 6027 hadi 5833.
Idadi ya kesi ziliripotiwa ni 111,822, ikiwa imeongezeka kwa 2,569 tangu Ijumaa.
Takwimu hizo zimetolewa na Jerome Salomon, Mkurugenzi Mkuu wa Afya wa Ufaransa.
Jumla ya watu 35,983 wamerudi nyumbani baada ya kupona kabisa.
Virusi hivi vilianzia China mnamo Desemba mwaka jana na kuenea katika nchi 185 duniani.
Virusi hivi vimeua watu zaidi ya 157,400 duniani kote na kuathiri watu zaidi ya milioni mbili.