Tuesday, April 21, 2020

MAKAHABA 24 NA WATEJA WAO WAKAMATWA WAKIJIVINJARI...KUWEKWA KARANTINI CORONA SIKU 14 KWA GHARAMA ZAO

Maafisa wa polisi kaunti ya Makueni nchini Kenya wamewakamata makahaba 24 pamoja na wateja wao wakiwa ndani ya hoteli moja mjini Emali wakijivinjari.

 Kulingana na ripoti ya polisi , makahaba hao walikamatwa kwa kosa la kuvunja amri ya kutokaribiana iliyotolewa na wizara ya Afya ili kudhibiti kusambaa kwa virusi vya corona. 

Washukiwa hao waliokamatwa Jumatatu, Aprili 20, watawekwa karantini ya lazima katika shule mbili za upili na watatakiwa kugharamia malipo yote.

Akithibitisha kisa hicho, Kamanda mkuu wa polisi kata ndogo ya Nzaui Josiah Dullo alisema makahaba hao walivunja sheria za COVID-19 na sharti wakabiliwe vilivyo. 

" Tumewakamata makahaba 14 wakiwa katika hoteli moja kule Kilungu wakiwa pamoja na wateja wao, tutawaweka karantini ya lazima kwa siku 14 na kisha baadaye tuwafikishikishe mahakamani," Dullo alisema.

Wahudumu wa baa hiyo waliokuwa wakiwauzia makahaba hao pombe pia walikamatwa na watajibu mashtaka dhidi ya kukiuka sheria za COVID -19. 

Washukiwa wote walipelekwa katika kituo cha polisi cha Emali kabla ya kupelekwa katika shule ya upili ya wasichana ya Mulala na ya wavulana ya Matiliku ambapo watatengwa kwa siku 14.
Chanzo - Tuko
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...