Sunday, July 7, 2019

Viongozi wa dini Watakiwa Kusimamia malezi ya Vijana ili kuhakikisha Taifa linakuwa na watu waliostarabika na kuwa na hofu ya Mungu.

NA SALVATORI NTANDU
Vijana hapa nchini wametakiwa kubadilika na  kuachana na vitendo vinavyomchukiza Mwenyezi Mungu ambavyo ni pamoja matumizi ya dawa za kulevya, wizi, na uasherati,  ambavyo vinaweza kubabisha wakapoteza mwelekeo na kutotimiza malengo yao

Kauli hiyo imetolewa leo  na kiongozi wa Vijana wa Kitaifa wa Jumuiya ya Waislam wa (Ahmadiya) Shekh, Ramadhani Hassani Nauja katika kongamano la siku tatu lijulikanalo kama Ijtemaa ya Khuddam kanda ya kaskazini la mwaka 2019 linalojumuisha washiriki kutoka mikoa saba lililofanyika katika wilaya ya kahama mkoani Shinyanga.

Amesema ipo haja kwa viongozi wa dini kuhakikisha wanawalea vijana katika misingi ya kiimani ambayo itawasaidia kupata thawabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu pamoja na kuwa raia wema katika maeneo wanayoishi.

Amesema vijana ndio nguvu kazi ya taifa hivyo ni budi kwa viongozi wa Dini wakawajengea misingi mizuri ya kumjua Mwenyezi Mungu na kuondokana na vitendo viovu kwani ndio kundi pekee ambalo lipo katika hatari kubwa ya kukumbwa na vishawishi katika ulimwengu huu.

Nae shekeh Musa Issa kutoka visiwani Zanzibar amesema viongozi wadini wapaswa kujikita kutoa elimu ya dini kwa wananchi waliopo vijijini ili kuwasaidia kumjua mungu na kuondokana na matukio ya mauaji  ya vikongongwe na ulawiti na watu wenye ualibo.

Kwa upande wake Shekhe Yusuph Mgeleka kutoka Kahama amesema Kongamano hilo litaweza kuwabadili vijana kifikra na kuwa raia wema kwa kufanya kazi halali ambazo zitaweza kuwapatia vipato na kuongeza nguvu kazi katika ukuaji wa uchumi wa taifa.

Mahdilah Issa na Musa Saidi ni miongoni mwawashiriki  Mafunzo hayo kutoka mikoa ya Tabora na Kagera wamesema mafunzo waliyoyapata yatawawezesha kuwa mabalozi kwa vijana wenzao katika maeneo yao wanayoishi ili kutoa fursa ya vijana wengine.

kongamano hilo limejumuisha vijana zaidi ya 200 kutoka katika mikoa ya Tabora, Mwanza, Kagera, Geita, Simiyu na Mara limeenda sambamba na mashindano ya Kusoma Quan tukufu,mashindano ya mpira wa miguu na shughuli mbalimbali za kijamii katika mji wa kahama na lilianza rasimi siku ya ijumaa na limehitimishwa hii leo.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...