Wednesday, April 10, 2019
CAG azibana CHADEMA, CCM kwenye ripoti
Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali, Prof. Mussa Assad, katika ukaguzi uliofanyika katika vyama vya siasa, CCM ilibainika kuwa haijawasilisha makato ya wafanyakazi wake.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mukhtasari wa kile kilichomo kwenye ripoti yake ya ukaguzi wa mwaka 2017/18, CAG amesema kwamba kiasi cha fedha cha shilingi bilioni 3.74 za wanachama wake.
Mbali na Chama Cha Mapinduzi, CAG ameeleza kwamba, "Tumebaini CHADEMA ilinunua gari jipya aina ya 'Nisan Patrol' kwa Sh milioni 147.5 lakini lililisajiliwa kwa jina la mwanachama badala ya Bodi ya Wadhamini.
Ameongeza kwamba gari hilo kwenye taarifa ya fedha ilioneshwa kwamba kama mkopo kwa mwanachama huyo bila kuwa na makubaliano ya mkopo yaliyosainiwa kati ya mwanachama huyo na bodi ya wadhamini wa CHADEMA.
Mbali na CHADEMA, CAG amesema kwamba pia wamebaini kuwa majengo ya ofisi za CUF yamesajiliwa kwa majina ya watu badala ya Bodi ya Wadhamini.
Mbali n ripoti ya vyama, CAG amesema katika ukaguzi wamebaini kwamba Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilinunua mashine za BVR 8000 kwa ajili ya usajili wa wapiga kura, mashine 5000 hazikukidhi vigezo na hivyo kutolandana kimatumizi na zile zilizonunuliwa awali na NIDA na RITA na kusababisha hasara ya Sh862.08m.
Hata hivyo ukaguzi wa CAG umebaini kwamba katika ukaguzi maalumu uliofanywa katika ununuzi wa sare za askari polisi uliofanywa na Jeshi la Polisi nchini, na kwamba walibaini kwamba jeshi lililipa Sh16.66 bn bila kuwepo kwa ushahidi wa uagizaji wala upokeaji wa sare hizo.
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Bongo Deco wauzai wa vifaa mbalimbali vya umeme kama TV, Subwoofer, Hometheator, Majiko madogo na makubwa ya Gesi, Friji, Generator nk leo w...
-
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia)akimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii wa Jamhuri ya ...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Kuongezeka kwa ghasia za hivi majuzi kumesababisha idadi kubwa ya raia wa Lebanon kukimbia kutoka Beirut huku milipuko ikitikisa jiji hilo...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Balozi mpya wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu akitoa hotuba yake kwa wageni mbalimbali waliohudhulia dhifa iliyoandaliwa maalum kwa kumk...
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekagua ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo – Busisi) ...
-
Wanajeshi wawili wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wamejeruhiwa baada ya kifaru cha Israel kufyatua risasi kuelekea mnara wa Umoja wa M...