Friday, March 22, 2019

Wanafunzi wa kike walia na wadau binafsi


Na. Rahel Nyabali,Tabora

Baadhi ya wanafunzi wa kike  walio katika mpango wa  TASSAF kwa lengo la  kunusuru kaya masikini unaoratibiwa na mfuko wa maendeleo ya jamii wamewaomba wadau binafsi, kushirikiana na serikali  ili kuweza kuwasaidia  kutimiza malendo yao.


Muungwana Blog ilifika katika baadhi ya shule hapa mjini Tabora ikiwemo shule ya sekondari Kazehili na kuzungumzana na baadhi ya wanafunzi walio katika mpango wa TASSAF ili kujua maendeleo yao kitaaluma.

Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Kazehii Marium Seif amesema wanafunzi wa kike walikuwa wanashindwa kuhudhuria darasani kutokana na kukosa mahitaji muhimu ya shule ikiwemo madaftari na sare za shule

"Mpango huu wa TASSAF umetusaidia kwa kiasi kwa sababu zamani  nilikua nakuja malamoja moja kwa wiki lakini baada ya kuwa katika mpango huu nahudhulia vizuri darasani ninawaomba wadau wengine wajitokeze kutusaidi," Amesema Marium.

 "Mwalimu mlezi wa wanafunzi katika shule ya sekondari Kazehili Sarah Misa amesema  wa wanafunzi  walio katika mpango wa TASSAF amesema mpango huu umekuwa na tija kwa  kwa kuongeza ufauru  hasa kwa wanafunzi wa kike."

"Tuna wanafunzi kama mia moja wanahudhuria katika shule yetu baada ya kuwa katika mpango huu wanafunzi wanahudhulia kwa asilimia tisini hakika hili ni jambo kubwa,"amesema Sarah.

Aidha mpango huu umejikita zaidi katika kusaidia kaya masikini pamoja na watoto  wanao ishi katika mazingira magumu ikiwemo Afya na Elimu ili kutimiza Malengo yao.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...