Saturday, February 9, 2019
Mollel Adai Kushambuliwa Lissu Kwa Risasi ni Mpango wa Chadema
Sakata la Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kushambuliwa kwa risasi limeendelea kuzua matamshi na mitazamo mbalimbali ambapo leo, Mbunge wa Siha, Dkt. Godwin Mollel (CCM) amesema kuwa ulikuwa mpango wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Dkt. Mollel ambaye alikuwa mbunge wa Chadema na baadaye kuhamia CCM ambako aligombea tena na kurejea bungeni akiwa amebadili chama, ameliambia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa yeye aliiba sampuli ambazo chama hicho kilimkataza kuzitumia.
Mbunge huyo amedai kuwa alipojaribu kuwasilisha sampuli hizo ili zipelekwe Afrika Kusini kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi alikataliwa na uongozi wa chama hicho kikuu cha upinzani kwa kile alichodai walifahamu kuwa wangeumbuka.
"Mimi nilikuwa huko lakini nilikimbia kwa mipango yao, hata katika tukio la kushambuliwa Lissu mimi niliingia ndani kwenye uchunguzi na niliiba baadhi ya vitu lakini walikataa mapendekezo yangu," alisema Mollel.
Hata hivyo, wabunge wa Chadema, Frank Mwakajoka (Tunduma) na Joseph Selasini (Rombo), kwa nyakati tofauti waliomba kutoa taarifa kuhusu hoja ya Mollel ambapo walimtaka mbunge huyo kuthibitisha kauli zake na kutovunja kiapo chake cha udaktari.
Akijibu kuhusu taarifa hiyo, Dkt. Mollel alidai kuwa ili athibitishe anataka Chadema waeleze wanakopeleka ruzuku za chama hicho pamoja na kile alichodai kuwa ni mpango wao dhidi ya Zitto Kabwe na marehemu Chacha Wangwe walipojaribu kugombea uenyekiti wa chama hicho.
Lissu amekuwa mjadala kwa nyakati tofauti ndani ya Bunge wiki hii kutokana na kauli anazozitoa hivi karibuni katika ziara zake za ughaibuni. Spika wa Bunge ameahidi kufanyia kazi hoja iliyowasilishwa na Mbunge wa Geita, Joseph 'Msukuma' Kasheku kuwa ofisi ya Bunge isitishe mshahara na stahiki za Lissu.
Mbunge huyo wa Singida Mashariki jana aliiambia Sauti ya Amerika kuwa anaendelea na matibabu na anatarajia kufanyiwa upasuaji wa 23 nchini Ubelgiji.
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Bongo Deco wauzai wa vifaa mbalimbali vya umeme kama TV, Subwoofer, Hometheator, Majiko madogo na makubwa ya Gesi, Friji, Generator nk leo w...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 29, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia)akimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii wa Jamhuri ya ...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Kuongezeka kwa ghasia za hivi majuzi kumesababisha idadi kubwa ya raia wa Lebanon kukimbia kutoka Beirut huku milipuko ikitikisa jiji hilo...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 15, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...