Monday, November 19, 2018

RC Makonda awapongeza Lulu na Majey


Lulu na Majey kwa sasa ni couple ambayo inatazwa zaidi kwa hapa Bongo kutokana na mahusiano yao kujaa utulivu wa aina yake.

Wawili hao kwa sasa wapo kwenye mipango ya kufunga ndoa na taarifa zilizopo ni zinadai kuwa hapo jana Majey alienda kutoa mahari kwa kina Lulu baada ya kumvisha pete ya uchumba.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambaye ni miongoni mwa wanakamati wa harusi hiyo ametia neno kile kichoendelea kwa sasa kati ya Majey na Lulu. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;

"Mafanikio yenu yamebeba watu wengi, na kila hatua inaonyesha hamtanii basi Mungu wangu aendelee kuwaonyesha njia ili mfikapo mkawe msaada na kwa wengine," ameeleza RC Makonda.

Utakumbuka August  18, 2018 kwenye Tamasha la Komaa, RC Makonda akizungumza na waandishi wa habari alisema, ' Majizo tayari yupo kwenye mipango na binti yangu Lulu na wameshakuja nyumbani na wameshafanya vikao vingi vya kupanga kwa ajili ya Harusi,'.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...