Sunday, November 18, 2018

Huu Hapa Mkoa Unaoongoza Kwa Kulima na Kutumia Bangi Tanzania


Serikali imewasilisha Bungeni jijini Dodoma taarifa ya hali ya #DawaZaKulevya nchini kwa mwaka 2017 ikionesha kuwa Mkoa huo unaongoza kati ya mikoa 8

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama alitoa taarifa hiyo jana na kuitaja mikoa mingine kuwa ni Arusha, Njombe, Tanga, Simiyu, Rukwa, Geita na Morogoro

Alisema kiasi cha bangi kilichokamatwa kilipungua kutoka tani 68.23 mwaka 2016 na kufikia tani 52.19 mwaka 2017 huku utumiaji wa Mirungi ukiongezeka kutoka tani 21.6 mwaka 2016 hadi kufikia tani 67.8 mwaka 2017

Idadi ya waliokamatwa na mirungi ilipungua kutoka 2,397 mwaka 2016 hadi 1,797 mwaka 2017 na hiyo ni baada ya wengi kukamatwa na kiasi kikubwa na baadhi ya mirungi kukamatwa bila wahusika baada ya kuitekeleza

Kiasi cha cocaine kilichokamatwa kilipungua kutoka kilo 18.52 mwaka 2016 hadi kufikia kilo 4.143 mwaka 2017 na hata Watuhuhumiwa waliokamatwa walipungua kutoka 263 mwaka 2016 na kufikia 243 kwa mwaka 2017

Aidha, alisema heroine iliyokamatwa nchini katika mwaka 2016 ilikuwa kilo 42.26 ikilinganishwa na kilo 185.557 zilizokamatwa 2017
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...