Wednesday, August 22, 2018

Mzozo wa Kidiplomasia Waibuka Kati ya China, Taiwan na Swaziland

Mzozo wa kidiplomasia waibuka kati ya China, Taiwan na Swaziland
Mzozo wa kidiplomasia unazidi kuibuka kuhusu nchi ndogo iliyo kusini mwa Afrika ya eSwatini ambayo awali ilifahamika kama Swaziland.

Nchi hiyo ndiyo mshirika wa mwisho wa Taiwan aliyesalia barani Afrika.

China ambayo hairuhusu nchi yoyote kuwa na uhusiano wa kiserikali nayo pamoja na Taiwan kwa wakati mmoja imesema inataka eSwatini kuboresha uhusiano kati yake na Beijing.

Taiwan ambayo China inaitaja kuwa mkoa wake, imekuwa ikipoteza washirika wakiwa sasa wamebaki 17 tu. Siku ya Jumanne El Salvador ilikata uhusiano wake na China.

Taiwan iliapa Jumanne kupambana na tabia za China baada ya kupoteza mshirika wake El Salvador kwa China, ambayo ni nchi ya tatu kukata uhusiano wake na Taiwan na kujiunga na China mwaka huu.


"eSwatini haina uhusianoa na China kwa sababu ambazo kila mtu anazifahamu," naibu waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa China Cheng Xiaodong aliliambia shirika la habari la Reuters.

"Tuna matumaini kuwa nchi zote za Afrika huku moja ikiwa imebaki, zitashiriki katika kuwa na uhusiano mzuri kati ya China na Afrika," alisema.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...