Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira imeitaka serikali kukaa na wamiliki wa viwanda nchini na kuhakiki gharama za uzalishaji ambazo zimekuwa zikisababisha bidhaa za wazalishaji wa ndani kushindwa kushindana na zinazoingizwa nchini.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Sadick Murad ametoa kauli hiyo jana Agosti 13, wakati kamati hiyo ilipotembelea kiwanda cha uzalishaji wa mabati na vifaa vingine Alaf.
Murad amesema gharama za uzalisha zimekuwa kikwazo kwa viwanda vya ndani ambazo vinazalisha bidhaa kwa bei ghali ilihali zinazoingizwa nchini zinauzwa kwa bei rahisi.
"Gharama za uzalisha zikiwa fair na wazalishaji wa ndani kupunguziwa kodi za umeme na tozo nyingine, gharama za uzalishaji zitashuka," amesema ambaye pia ni Mbunge wa Mvomero (CCM).
Aidha, alitoa wito kwa wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji, kuisimamia vema Shirika la Viwango (TBS) na Mamlaka ya Mapato (TRA) ili ziendelee kutoa huduma rafiki kwa wazalishaji wa ndani ambao wamekuwa chachu katika uzalishaji wa ajira na ukuzajia uchumi.
Hata hivyo, Katibu mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Profesa Joseph Buchweshaija amesema tayari imeandaa mpango maalumu wa kwa kushirikiana na TBS kuondoa bidhaa hafifu sokoni. Tayari tumeanza kuisafisha suala hilo na ninawaahidi kuendelea kutekeleza yote mliyoagiza," amesema.
Aidha, Meneja Mkuu wa kiwanda hicho cha Alaf, Dipti Mohanty aliieleza kamati hiyo kuwa umeme umeendelea kuwa mojawapo ya kikwazo kikubwa katika uzalishaji wa bidhaa zao.
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Bongo Deco wauzai wa vifaa mbalimbali vya umeme kama TV, Subwoofer, Hometheator, Majiko madogo na makubwa ya Gesi, Friji, Generator nk leo w...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia)akimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii wa Jamhuri ya ...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Kuongezeka kwa ghasia za hivi majuzi kumesababisha idadi kubwa ya raia wa Lebanon kukimbia kutoka Beirut huku milipuko ikitikisa jiji hilo...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 15, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekagua ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo – Busisi) ...