Friday, November 22, 2024

Baada ya Kuonekana na Wachezaji wa Yanga, Fredy Funga Funga Amwaga Wino Huku

 

Baada ya Kuonekana na Wachezaji wa Yanga, Fredy Funga Funga Amwaga Wino Huku

BAADA ya kutambulishwa rasmi na Zesco United, aliyekuwa mshambuliaji wa Simba SC, Freddy Michael Koublan, amejipanga kurejea kwa kishindo kwenye soka la ushindani.

Mshambuliaji huyo kutoka Ivory Coast, anarejea kwenye Ligi Kuu ya Zambia baada ya kupita takribani miezi 11 tangu aondoke Green Eagles Januari 2024 na kutua Simba.

Freddy aliyeitumikia Simba kwa kipindi cha miezi sita akifunga mabao manane katika mechi 13, amejiunga na Zesco United kwa mkataba wa mwaka mmoja baada ya kukaa kwa muda bila ya timu.

"Nilifurahia maisha yangu ya soka Tanzania na nilikuwa na nafasi ya kuendelea kucheza huko kutokana na timu ambazo zilivutiwa na mimi lakini nashukuru Zesco kwa imani kubwa zaidi waliyoonyesha juu yangu," alisema mshambuliaji huyo.

Taarifa rasmi iliyotolewa na Zesco United, ilisema: "Zesco United Football Club ina furaha kutangaza usajili wa mshambuliaji wa kimataifa kutoka Ivory Coast, Freddy Michael Koublan, kwa mkataba wa mwaka mmoja."

Freddy wakati anatua Simba dirisha dogo msimu uliopita 2023-24, aliondoka katika Ligi Kuu ya Zambia akiwa na mabao 14 yaliyomfanya kuongoza orodha ya wafungaji kunako ligi hiyo.

Akizungumzia malengo yake akiwa na Zesco United, Freddy alisema: "Nina kazi kubwa ya kufanya, na naamini tutafikia mambo makubwa msimu huu. Kama mnavyonijua, mimi ni mtu wa malengo na nipo hapa kutoa mchango wangu."

Kocha wa Zesco United, George Lwandamina, alizungumza kuhusu usajili wa Freddy kwa kusema: "Freddy ni mchezaji mwenye uzoefu mkubwa na historia nzuri ya kufunga mabao. Tunamuhitaji sana katika safu yetu ya ushambuliaji, na tunaamini atatusaidia kutimiza malengo yetu."

MNEC ASSAS AELEZA MKAKATI WA CCM KATIKA VITUO 87,000 VYA KUPIGIA KURA


Ruvuma. Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (MNEC), Salim Abri Assas, ameweka wazi mikakati ya chama hicho kuelekea uchaguzi wa mwaka 2024, akibainisha kuwa vituo vyote 87,000 vya kupigia kura nchi nzima vitakuwa na sanduku la kura, hata katika maeneo ambayo hayana wagombea wa vyama vya upinzani.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni mkoani Ruvuma, Assas alisisitiza umuhimu wa wanachama wa CCM kushiriki kwa wingi katika mchakato wa uchaguzi. "Tutahakikisha kila kituo kina sanduku la kura, na pale ambapo hakuna wagombea wa upinzani, wapiga kura watapiga kura za ndiyo kuwachagua viongozi bora wa CCM," alisema.

Katika hotuba yake, Assas alisisitiza umuhimu wa mshikamano wa wanachama wa CCM, akieleza kuwa mafanikio ya chama hicho yanatokana na juhudi za pamoja za wanachama wake. "Tunataka kuhakikisha viongozi wanaochaguliwa wanadumisha misingi ya maendeleo na mshikamano wa kitaifa," aliongeza.

MNEC Assas alitumia fursa hiyo kuhimiza wananchi kuendelea kuamini katika CCM kama chama chenye dira ya maendeleo, akitaja miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa nchini kuwa ushahidi wa mafanikio yao.

Wanachama wa CCM waliojumuika kwenye mkutano huo walionyesha shauku kubwa, wakiahidi kushiriki kikamilifu katika kuhakikisha chama hicho kinaendelea kuwa mtetezi wa maendeleo ya taifa.

CMSA yazindua mfuko wa uwekezaji wa M-WEKEZA ''mteja atapata faida hadi 13%''


MAMLAKA Ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA,) imezindua rasmi mfuko wa uwekezaji wa M-WEKEZA ambao ni mradi wa pamoja wa kampuni ya Sanlam Investments East Africa Limited na M-PESA Limited ikiwa ni hatua muhimu katika maendeleo ya sekta ya fedha hususani masoko ya mitaji katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa kuzinduliwa kwa jukwaa hilo Afisa Mtendaji Mkuu wa CMSA CPA. Nicodemus Mkama amesema uzinduzi wa jukwaa hilo utaimarisha na kuongeza kasi ya malengo ya kuwawezesha kifedha wafanyabiashara binafsi katika ukanda wa Afrika na kupitia M-WEKEZA jukwaa la uwekezaji kwa njia ya simu litawawezesha watu binafsi kupata fursa ya uwekezaji kwa urahisi katika maeneo ya mijini na vijijini kwa kutoa huduma za kifedha.

''Kupitia M-Wekeza mteja anaweza kuwekeza Kiwango chochote na kupata faida mpaka 13% endapo atawekeza fedha zake kwa mwaka mzima na unaweza pata taarifa ya kifedha ya uwekezaji wake muda wowote kiganjani mwake'' amesema.

Ameongeza kuwa mpango huo unatoa fursa za uwekezaji kwa wawekezaji wakiwemo wanawake na vijana hali itakayochagiza maendeleo kwa kuhamasisha akiba ya ndani kupitia uwekezaji, kutengeneza fursa za ajira na kujenga uchumi thabiti wa Taifa.

Aidha uzinduzi wa jukwaa hili pia unaendana na mfumo wa tatu wa kitaifa wa ujumuishaji wa kifedha wa 2023/2028 ambao unasisitiza matumizi ya kidigitali katika usambazaji na utoaji huduma za kifedha."Amesema.

Pia ameipongeza menejimenti ya Sansalam Investment East Africa Limited na M-PESA Limited kwa jitihada za kuunganisha mifumo yao na kupata kibali cha CMSA ambayo imeendelea kuweka mazingira rafiki ya kisera, udhibiti na utendaji yanayochagizwa na uimara wa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

"Kazi kubwa ya masoko ya mitaji ni kukusanya rasilimali kutoka kwa wawekezaji na kuzielekeza kwenye uwekezaji wenye tija na kuchochea maendeleo katika Serikali, mamlaka za mitaa, taasisi kubwa na ndogo na kampuni mbalimbali ambazo hutoa fedha zinazoelekezwa katika miradi mbalimbali ya maendeleo,"amesema CPA Mkama.

Afisa Mtendaji Mkuu wa CMSA CPA. Nicodemus Mkama akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mfuko wa uwekezaji wa M-WEKEZA ambao ni mradi wa pamoja wa kampuni ya Sanlam Investments East Africa Limited na M-PESA Limited
 





Thursday, November 21, 2024

Yanga Kumsajili Mshambuliaji Huyu Kutoka Uganda...Noma na Nusu


YANGA imeanza mikakati ya kuimarisha safu yake ya ushambuliaji katika dirisha dogo la usajili litakalofunguliwa Desemba 15 mwaka huu ambapo jina la mshambuliaji Bayo Aziz Fahad ndio kipaumbele chao cha kwanza.

Bayo mwenye umri wa miaka 26, inaripotiwa kuwa ameshafanya mazungmzo na kumalizana na vigogo wa Yanga ambapo wamefikia pazuri huku kilichobaki kwa mchezaji huyo ni kusubiri dirisha dogo ili ajiunge nayo.

Uwezo wa kufunga na kupiga pasi za mwisho ambao Bayo amekuwa nao unaonekana kuiridhisha Yanga ambayo ujio wa mshambuliaji huyo utasaidia safu yake ya ushambuliaji lakini pia kuwaongezea ushindani chanya washambuliaji waliopo kikosini ambao wanaonekana bado wanajitafuta.

Kwa sasa, Bayo ni mchezaji huru baada ya kuachana na MFK Vyskov inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Czech ambayo aliichezea mechi 42 na kuifungia mabao manane.

Kabla ya kujiunga na Vyskov, Bayo aliitumikia Ashdod inayoshiriki Ligi Kuu ya Israel ambako katika mechi 41 alizoichezea, alifunga mabao manane huku akipiga pasi moja ya mwisho.

Katika timu ya taifa ya Uganda, mshambuliaji huyo amecheza mechi 21 na kuhusika na mabao tisa, akifunga mabao manane (8)
.

Australian and Tanzanian mining partnerships worth over TZS 10 trillion


Australian investment in Tanzania is expanding, with mining contracts signed in the past two years with Australian companies valued at over TZS 10 trillion (USD 3.6 billion).

The Australian and Tanzanian mining sector came together today in Dar es Salaam for a breakfast and panel discussion hosted by the Australian Deputy High Commissioner Chris Ellinger and Australian Trade and Investment Commissioner for Africa Scott Morriss who are in the country for the Tanzania Mining and Investment Conference.

Joined by Deputy Minister of Minerals, the Hon. Dr. Steven L. Kiruswa MP, the panel discussion explored the significant potential for Australian investment in Tanzania, with mines moving into construction phase as well as opportunities within the subsequent value chain. The Deputy Minister highlighted the Tanzanian Government's openness for consultation on potential projects, and that Australian technology and training avenues are assisting to grow Tanzania's mining value chain.

Australia-Africa ties are expanding with Australian companies investing over AUD $60 billion in mining projects across Africa. In Tanzania, 35 Australian companies have invested in mineral exploration, mining, value addition and geohazard management while applying the highest Environmental, Social, and Governance standards. New research from the Australian Government indicates that twelve Australian companies set aside approximately USD $26 million for exploration in Tanzania - a practical demonstration of Australia's confidence in, and commitment to, the future of mining in Tanzania.

In September 2024, Tanzanian Minister of Minerals Anthony Mavunde was an official guest at Africa Down Under, Australia's most significant Africa-focused mining conference, where he held bilateral talks with Australia's Assistant Minister for Foreign Affairs the Hon. Tim Watts MP. Tanzania's Commissioner for Minerals, Dr Abdul Mwanga, is currently in Australia undertaking further mining-related university studies under the Australia Awards program.

Australian Trade and Investment Commissioner for Africa Scott Morriss said:
"Australian companies are providing education and skills opportunities to local African communities around mining operations, and over 65 per cent of Australian Mining, Equipment Technology and Services (METS) companies export to overseas mining destinations including a third to Africa. These companies have established strong resilient supply chains globally that can flexibly adapt to customer needs."

Deputy High Commissioner Chris Ellinger said:
"Tanzania's mining sector has consistently contributed significantly to the country's GDP. From 2018 to 2022, the sector's contribution grew from 4.8% to 9.1% and the Tanzanian Government aims to increase the mining sector's contribution to 10% of GDP by 2025. Australia's world class expertise in the resources sector makes us an important partner for Tanzania and we look forward to seeing Australian-facilitated investments delivering more jobs, skills and revenue to Tanzania in the future."

WENYE MATATIZO YA KIAFYA KUPEWA KIPAUMBELE KUPIGA KURA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Hemed Suleiman Abdullah   
Na Hadija Bagasha Tanga, 

Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Hemed Suleiman Abdullah, amewataka viongozi wa Mkoa wa Tanga kuhakikisha watu wenye matatizo ya kiafya, ambao hawana uwezo wa kufika vituoni kupiga kura, wanapatiwa usafiri ili kuhakikisha kila mtu anashiriki zoezi hilo kikamilifu. 

Hatua hii inalenga kuhakikisha kila mmoja anashiriki kikamilifu katika zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa, kwa maendeleo ya nchi yao.

Pia Serikali imewatoa hofu wananchi kuwa uchaguzi wa Serikali za mitaa kuwa utafanyika Kwa salama na amani na atakae jaribu kuleta chokochoko atachukuliwa hatua Kali za kisheria.

Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu mlezi wa chama hicho , Hemed Suleiman amesisitiza umuhimu wa ushiriki wa wananchi wote katika uchaguzi huo huku  akiungwa mkono na mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajabu Abrahman Abdallah. 

"Kwenye hili lazima wapo viongozi wakae mbele kuona kila eneo kila nyuma kuangalia nani ameenda kupiga kura na ambaye hajakwenda kujua sababu gani pengine afya yake sio nzuri apelekewe usafiri aende kupiga kura tusikubali tukamwacha mtu yeyote bila kupiga kura niwahakikishie nchi yetu itaendelea kuwa salama kura zitapigwa kwa amani kabisa,"alisisitiza Makamu wa pili wa Rais.

Alisema kuwa serikali imejipanga kuimarisha usalama na amani Ili wananchi waweze kushiriki vizuri katika uchaguzi na kuendelea na majukumu yao.

"Watanzania niwaondoe wasiwasi uchaguzi huu ni salama ila niwaonye wale ambao wanania ya kuuharibu basi hatutasita kuwachukulia hatua"alisema Makamu wa Rais 

Aidha alivitaka vyama kuendesha kampeni za amani bila ya vurugu wala matusi kwani sifa za watanzanzia ni kudumisha amani.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajab Abrahman alisema kuwa katika ya vijiji 763 wapinzani wamesimamisha wagombea katika vijiji 140 pekee hivyo hiyo inatupa matumaini ya kushinda Kwa kishindo katika uchaguzi huu.

Aidha, baadhi ya wananchi walioshiriki mkutano huo walionyesha msisitizo wa kushiriki kwenye uchaguzi kwa kusema kuwa ni fursa ya kuchangia maendeleo ya taifa.

Ushiriki wa wananchi wote, bila kujali hali zao za kiafya au mazingira, ni muhimu kwa kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa haki na jumuishi, Viongozi wa mkoa wanatakiwa kutekeleza jukumu lao la kuwezesha usafiri kwa wale walio na changamoto ili kuhakikisha kila mmoja anatimiza haki yake ya kikatiba.


Airtel Africa-UNICEF Partnership Connects 1,200 Schools, 1m Africa Children to Digital Education


Africa, 20 November 2024: Airtel Africa, a leading provider of telecommunications and mobile money services across 14 African countries, has today announced that its five-year partnership with United Nations Children's Fund (UNICEF), aimed at transforming education across the continent, has connected over 1,500 schools to the internet, trained 17,000 teachers, and reached nearly a million learners with quality digital education resources across 13 African countries.

The partnership was launched in 2021 as part of Airtel Africa's $57 million commitment to support the development of education and bridge the digital divide for vulnerable children in remote communities in collaboration with African governments.

Since the commencement of the partnership, Airtel Africa has prioritised the accessibility of online learning resources, including zero-rated educational platforms and teacher training, to support equitable learning opportunities for Africa's children.
Airtel Africa CEO, Sunil Taldar, speaking on the success of the partnership while marking this year's World's Children's Day said: 

"Our mission is to transform lives, and through our collaboration with UNICEF, we are witnessing the profound impact that connectivity and digital resources can have on Africa's children and teachers. For every school we have connected and for each teacher trained on using these digital tools, we are taking tangible steps toward realizing our commitment to bridging the digital divide, advancing educational equality and restating our commitment to the relentless pursuit of a better future for African children on the continent.

According to Mr. Taldar, "by equipping these schools with internet connectivity and training teachers on how to use the digital tools, Airtel Africa and UNICEF are providing Africa's children, particularly those in underserved and remote regions, with the digital tools and skills they need to thrive in a technology-driven world.

This is why we are celebrating with the children on this special occasion of World Children's Day, specially dedicated to them and all the effort aimed at securing and improving their future.
The partnership has expanded digital learning to learners in 13 countries since its launch. The countries include Chad, Congo, Democratic Republic of Congo, Gabon, Kenya, Madagascar, Malawi, Niger, Nigeria, Rwanda, Tanzania, Uganda, and Zambia.

Wednesday, November 20, 2024

Stars Kufuzu AFCON Rais Samia Kaingia Kwenye Historia

Stars Kufuzu AFCON Rais Samia Kaingia Kwenye Historia

Stars Kufuzu AFCON Rais Samia Kaingia Kwenye Historia


Tanzania inang'ara katika mwanga wa uongozi thabiti wa Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye ameonyesha dhamira ya dhati ya kuimarisha umoja, kukuza uzalendo, na kusherehekea mafanikio ya kitaifa.

Siku ya jana, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam ulijaa furaha na fahari kubwa, huku Watanzania wakikusanyika kwa wingi kushuhudia Taifa Stars ikifanikisha hatua ya kihistoria ya kufuzu kwa AFCON 2025.

Tukio hili halikuonyesha tu mafanikio ya timu yetu ya taifa, bali pia athari chanya za uongozi wa Rais Samia.

Ushindi Ndani na Nje ya Uwanja

Chini ya uongozi wa maono wa Rais Samia, Tanzania imepiga hatua kubwa.

Kufaulu kwa Taifa Stars kufuzu kwa AFCON 2025 ni ushahidi wa jinsi Rais alivyojitoa kuimarisha michezo na kuendeleza roho ya ushindani wa hali ya juu.

Hata hivyo, mechi dhidi ya Guinea ilikuwa zaidi ya mchezo wa mpira—itakuwa kumbukumbu ya mshikamano wa kitaifa wa Watanzania.

Hatua ya Rais kulipia kiingilio na kugawa bure jezi za Taifa Stars zilizopambwa na picha yake imepokelewa kwa shangwe kubwa.

Zaidi ya mashabiki 65,000 walijazana uwanjani, wakizidi uwezo wa viti 60,000 vya uwanja huo. Taswira ya maelfu ya mashabiki wakiwa wamevaa jezi zinazofanana, wakiongozwa na upendo wao kwa taifa na shukrani kwa ukarimu wa Rais, ilikuwa ya kufurahisha na ya kutia moyo.

Jezi na Kiingilio Bure: Ishara ya Mshikamano

Hatua ya kugawa jezi bure zenye picha ya Rais Samia na kuondoa gharama za kiingilio si msaada wa kifedha pekee—ni ishara ya dhamira ya Rais ya kujumuisha kila mtu na kujenga uhusiano wa karibu na wananchi.

Hatua hii thabiti ilihakikisha kuwa Watanzania wa hali zote walipata fursa ya kushiriki tukio hili la kihistoria.

RAIS DKT. SAMIA ATEMBELEA ENEO LILIPO POROMOKA GHOROFA KARIAKOO..AWAJULIA HALI MAJERUHI MUHIMBILI



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimjulia hali na kumpa pole mmoja wa majeruhi wa ajali ya kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo ambao wamelazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), Ilala Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Novemba, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akikagua eneo la maafa ya ajali ya kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Novemba, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akikagua eneo la maafa ya ajali ya kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Novemba, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi mara baada ya kukagua eneo la maafa ya ajali ya kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Novemba, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi mara baada ya kukagua eneo la maafa ya ajali ya kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Novemba, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwajulia hali na kuwapa pole majeruhi wa ajali ya kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo ambao wamelazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), Ilala Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Novemba, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwajulia hali na kuwapa pole majeruhi wa ajali ya kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo ambao wamelazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), Ilala Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Novemba, 2024.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...