Wednesday, August 21, 2024

Mbinu tatu (3) za Kumtongoza Msichana ili Akubali Mapema

 

Mbinu tatu (3) za Kumtongoza Msichana ili Akubali Mapema

 Mbinu tatu (3) za Kumtongoza Msichana ili Akubali Mapema

Miongoni mwa maswali ambayo huwachanganya wavulana wengi ni pamoja ni kwa jinsi gani anaweza kumtongoza msichana na hatimaye akakubali. Wengi wao wanakuwa hawana ile nguvu ya kujiamini  ya kumtongoza msichana huyo macho kwa macho, wengi wao utawasikia ooh samahani naomba namba yako.


Sasa ili kuwaponya madomo zenge walio wengi hii ndiyo tiba ya kumtongoza mrembo yeyote hatimaye akakukubali.


1. Usimfanye ajue unampenda kwa dhati.


Wanaume wengi huwa wanafanyaga kosa hili kubwa . Wanawaambia wanawake wanawapenda au wanahisia za kimapenzi kwao . Ni kweli unampenda , anajua hivyo tayari . Au hajui ? Unampigia simu kila saa , mnataniani kimapenzi na anaona uhusiano wenu kabisa .


Kwahiyo japokua anahisi unampenda , usije kuonyesha hivyo kwani anahitaji kusikia kutoka kwako ili ajihakikishia hisia zake . Chukulia poa na usifunguke kuhusu hisia zako kwake , kitendawili alichonacho ndicho kitamfanya azidi kukunata na kutaka kujua mwisho wa mambo .


2. Ishi Maisha mawili


Unapoongea nae usiku , mwaga sera zako na funguka kuhusu mambo ya mapenzi sema mkikutana ana kwa ana mchana usiongelee mambo ya mapenzi kabisa labda aanze yeye na hivyo kumaanisha ashaingia line na anapenda maongezi hayo .


Pia epuka kuongelea kuhusu mambo yenu ya kimapenzi mnapokua na marafiki wengine bali fanyeni hivyo mkiwa wawili . Kwa kufanya hivyo unamfanya aamini kuna uhusiano motomoto wa siri unapikika kati yenu


3. Kuwa karibu na mtu huyo.

Siku zote , kama unataka kumtokea msichana njia muhimu kabisa ni kuweza kumjua kwa undani .Usikurupuke kurupuke tu ukaanza kutongoza , msichana ataogopa au atakuona mtu rahisi kua nae na mwisho wa siku utaishia kumboa tu .


Ongea nae na upate kumjua vizuri . Mtumie message na usiwe na mzuka , mfanye awe kama rafiki kwanza . Usimtokee kwanza sema pia usisubiri sana maana ataanza kukuchukulia poa .


Ukitumia mbinu hizo tatu nina imani kubwa ni lazima msichana huyo utampata tu.

Tuesday, August 20, 2024

VIDEO: Tunataka 'afande' afikishwe mahakamani-TLS


Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) kimelitaka Jeshi la Polisi kumfikisha mahakamani mtu aliyetambulika kwa jina la 'afande' ambaye anadaiwa kuwatuma vijana wanne waliohusika kumbaka na kumlawiti binti kisha video hizo kusambaa mitandaoni.

Akizungumza na vyombo vya Habari, rais wa TLS, Boniface Mwabukusi amesema mtu huyo aliye nyuma ya tukio hilo amehusika kwenye uhalifu huo hivyo afikishwe mahakamani mara moja, huku akieleza kuwa TLS itafuatilia kwa ukaribu shauri hilo ili binti huyo apate haki yake.

"Tunataka aliyesababisha kitendo kile kufanyika na yeye ni mkosaji, afikishwe mahakamani mara moja. TLS itaona namna bora ya kuweka wakili atakayekuwa akifuatilia ili kuona maendeleo ya shauri lile yatakavyokuwa yakiendelea na kuhakikisha kuwa haki za binti yule hazipotei," amesema Mwabukusi.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI.......USISAHAU KUSUBSCRIBE

Sunday, August 18, 2024

Friday, August 16, 2024

TANZANIA IPO TAYARI KUTUMIA FURSA YA SOKO LA PAMOJA KUUZIANA UMEME - DKT. BITEKO


Na Mwandishi wetu, Kampala, Uganda

Tanzania imejipanga vema kuhakikisha inatumia fursa ya uwepo wa soko la pamoja la mauziano ya umeme kwa nchi wanachama wa soko la pamoja la nchi za Mashariki mwa Afrika (East African Power Pool)- EAPP kwa kuhakikisha inaunganisha miundombinu yake ya kusafirisha umeme na nchi wanachama wa EAPP.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko wakati wa mkutano wa 19 wa nchi wanachama wa umoja wa mauziano ya umeme EAPP uliowakutanisha Mawaziri wa Nishati na Makatibu Wakuu nchini Uganda.

Mkutano huo umezungumzia masuala mbalimbali ikiwemo kupitisha mabadiliko ya muundo wa kiuongozi wa EAPP, kuridhia kanuni na taratibu za kiuendeshaji za EAPP sambamba na kuridhia uwepo wa kitengo huru cha masoko kinachojitegemea kusimamia soko la pamoja la mauziano ya Umeme kwa nchi wanachama.
'"Nafurahi kuona kuwa tumefikia muafaka kwenye masuala ya msingi kwenye kikao cha Mawaziri wa Nishati hususani uwepo wa kitengo huru cha Masoko kinachojitegemea kwa ajili ya kusimamia mauziano ya umeme na kwakuwa Tanzania tutakuwa na umeme kutoka mradi wa bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere -JNHPP, tutatumia vema fursa hiyo kuwauzia umeme nchi wanachama pale tutakapokuwa na ziada na sisi kununua tutakapokuwa na upungufu'' amesema Dkt. Biteko.

Katika kufanikisha hilo Dkt. Biteko amesema tayari miundombinu wezeshi inaendelea kuwekwa kupitia Shirika la Umeme Tanzania TANESCO ili kujiandaa kuingia kwenye soko la pamoja ambapo laini kubwa ya kuunganisha Tanzania na Kenya kupitia Namanga imeshajengwa na imekamilika na ile ya kuunganisha Tanzania na Zambia- TAZA imeshaanza kujengwa na itakamilika ifikapo 2026.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa sasa wa soko la pamoja la kuuziana umeme la nchi za kaskazini Mashariki EAPP na Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini nchini Uganda Mhe. Dkt. Ruth Ssentamu amesema EAPP imeridhia ushiriki wa Makatibu Wakuu wa Nishati kutoka nchi wanachama kushirikishwa katika muundo wa kiutawala wa EAPP kwa ajili ya kusaidia kuchakata na kupitia taarifa kutoka kwa watendaji wa kisekta kabla ya kupelekwa katika kikao cha baraza la Mawaziri la nchi wanachama ili kutolewa maamuzi.
Aidha, Mhe Ssentamu amesema maadhimio hayo yamefikiwa kufuatia makubaliano ya mkutano wa 18 wa baraza la mawaziri ulioanyika nchini Kenya kuhusu umuhimu wa kupitia mapendekezo ya uendeshaji wa shughuli za EAPP.

Naye, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Mha. Felchesmi Mramba amesema pindi uuzaji wa umeme kwenye soko la pamoja utakapoanza utatoa nafasi za ajira kwa nchi wanachama wa EAPP pamoja na kubadilishana wataalamu hususan kwenye miradi ya kusafirisha umeme na hivyo kuiongezea TANESCO mapato na hatimae kutoa nafasi ya ukuaji wa pato la Taifa.

Ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo wa Baraza la Mawaziri wa Nishati uliongozwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. Dennis Londo, Katibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Mha. Felchesmi Mramba, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Mha. Gissima Nyamo-Hanga, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Mipango, Utafiti na Uwekezaji TANESCO CPA Renata Ndege, viongozi waandamizi kutoka Wizara ya Nishati na Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.





Waziri wa fedha kuweka jiwe la msingi ujenzi wa chuo cha Uhasibu kampasi ya Babati.

Na John Walter -Babati 

Waziri wa fedha Dkt Mwigulu Nchemba anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika chuo cha Uhasibu Arusha tawi la Babati mkoani Manyara kuweka jiwe la msingi ujenzi wa chuo hicho awamu ya kwanza.

Taarifa iliyotolewa na Meneja wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kampasi ya Babati, Dr Eliakira Nnko, Dkt Nchemba anatarajiwa kufika chuoni hapo Agosti 22,2024.

Akieleza kuhusu ujenzi wa chuo hicho, Dr Nnko amesema majengo ya hosteli yamefikia asilimia 75 ya ujenzi wake na gharama yake ni shilingi  Bilioni 4.

Jengo la taaluma na ofisi za Wanafunzi ambalo lipo katika hatua za mwisho za umaliziaji gharama yake ya Ujenzi ni shilingi bilioni 5, bwalo la chakula shilingi bilioni 1 na kwa sasa limefika asilimia 45 ya ujenzi.

Dr Nnko ameeleza kuwa ujenzi wa majengo hayo wanatumia mfumo wa malipo wa Force account kupitia mafundi wa kawaida ambao hutumia gharama ndogo ukilinganisha na kutumia wakandarasi.


Amesema Wanafunzi wanatarajiwa kuanza kuingia chuoni hapo kuanzia Mwezi wa 10, 2024 mwaka wa masomo unapoanza. 

Aidha chuo hicho kina uwezo wa kupokea Wanafunzi 2500 hadi 2700.

Mkuu wa mkoa wa Manyara Mheshimiwa Queen Sendiga amefika chuoni hapo kuangalia maandalizi ya mapokezi ya mgeni huyo wa kitaifa akiwapongeza kwa usimamizi wa ujenzi wa awamu ya kwanza.

DC- Ndemanga awataka wawekezaji wa ndani kusajili kazi zao.



Na Ahmad Mmow,  Lindi.


Katika kuhakikisha kunakuwa na kumbukumbu sahihi za kazi na shughuli zinazofanywa na wawekezaji wa ndani. Wametakiwa kusajili kazi na shughuli wanazofanya kwa mujibu wa sheria.


Wito huo ulitolewa jana mjini Lindi, na mkuu wa wilaya ya Lindi,  Shaibu Ndemanga wakati wa semina ya uhamasishaji uwekezaji wa ndani iliyoandaliwa na kituo cha uwekezaji nchini(TIC).


Ndemanga  alitoa wito kwa wafanyabiashara na wawekezaji kusajili kazi na shughuli zao za kiuchumi ili zitqtambulike na serikali. Kwani wataweza kuzijua na kupata fursa mbalimbali.


Ndemanga ambae katika semina hiyo alimuwakikisha mkuu wa mkoa wa Lindi na  kuyashirikisha makundi mbalimbali ya wafanyabiashara, wawekezaji wadogo, taasisi za serikali, taasisi za fedha na waandishi wa habari alisisitiza kuwa ni muhimu Kwa wananchi, hasa  wazawa wakiwamo wa mkoa wa Lindi kuwekeza zaidi katika miji yao ili wasaidie upatikanaji wa ajira kwa vijana wazawa. Huku akibainisha kwamba ni vigumu kwa wawekezaji wa nje kutoa kipaumbele cha kuajiri wazawa badala yake fursa  zinapelekwa Kwa raia wa nchi zao.


Kwa upande wake ofisa uhamasishaji wa kituo cha uwekezaji Tanzania, Felix John, alifafanua kwamba umuhimu wa kupata usajili wa biashara kutoka katika Kituo hicho ikiwa ni pamoja na kuwa na takwimu sahihi zinazosaidia kutoa taarifa katika mamlaka mbalimbali zinazohusika na sekta ya biashara na uwekezaji.  Lengo likiwa ni kusaidia kuratibu mipango endelevu ya kiuchumi.


TIC imeendesha semina ya uhamasishaji uwekezaji wa ndani kwa wafanyabiashara ikiwa ni awamu ya pili baada ya kuzindua Septemba 25, mwaka jana 2023.

Thursday, August 15, 2024

DEREVA,UTINGO NA ABIRIA WATEKETEA KWA MOTO AJALI MALORI KUGONGANA USO KWA USO KAHAMA


Dereva,Utingo na abiria wamefariki dunia kwa kuteketea kwa moto huku wengine watatu wakijeruhiwa katika ajali iliyohusisha Malori mawili kugongana uso kwa uso katika eneo la Manzese wilayani Kahama mkoani Shinyanga huku chanzo cha ajali hiyo kikitajwa kuwa uzembe na Mwendokasi.
Inaelezwa kuwa ajali hiyo imehusiha malori mawili ya mizigo  ambapo baada ya kugonga uso kwa uso  yalianza kuwaka moto  na kusababisha vifo vya dereva, utingo na mtu mwingine ambaye anaidawa kuwa ni abiria ambapo jina lake bado halijafahamika.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambayo imehusisha Malori mawili ya Mizigo Namba T 854 DBY lenye tela namba T 180 DVH na Lori namba T 195 EEY lenye tela namba T 811 DYU. #Malunde 1 blog Updates

Tatizo Simba Sio Straika

 

Tatizo Simba Sio Straika

Hakuna asiyejua kama Simba kwa sasa ni mpya. Timu hiyo iliyomaliza nafasi ya tatu msimu uliopita imeundwa upya. Ina benchi jipya kabisa la ufundi chini ya Fadlu Davids.


Imesajili wachezaji wapya 13. Ni zaidi ya kikosi kizima kuonyesha kwamba Simba kwa sasa ndo kwanza inaanza kujitafuta.


Kumbuka ni wiki kama mbili tu, imetoka kambini huko Ismailia, Misri ilikoenda kujifua kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa mashindano wa mwaka 2024-25.


Tangu timu hiyo ilipoenda kambini hadi iliporudi nchini, imecheza mechi sita tu zikiwa ni nne za kirafiki na mbili za kimashindano, ikiendelea kutafuta muunganiko.


Imechezesha mechi tatu za kirafiki za kujipima nguvu ikiwa Ismailia, Misri na kocha Fadlu alikaririwa akiwasifia wachezaji kwamba wameanza kumpa mwanga na pia kujisifia kwa kutopoteza mechi yoyote kati ya ilizocheza.


Ilianza kwa kuifunga Canal SC kwa mabao 3-0, kisha kushinda 2-1 dhidi ya Telecom Egypt na Al Adalah ya Saudia kwa idadi kama hiyo ya 2-1, kisha timu iliporejea nchini, imecheza mechi moja ya kirafiki katika Tamasha la Simba Day dhidi ya APR na kushinda mabao 2-0. Ulikuwa mwanzo mzuri, yaani mechi tatu mabao saba na kufungwa mawili, sio uwiano mbaya kwa timu inayojitafuta, hata kama haikucheza dhidi ya timu ngumu.


Ndipo sasa ikacheza mechi mbili za kimashindano ya Ngao ya Jamii 2024, ikianza dhidi ya Yanga na kulala 1-0 kabla ya kupata ushindi wa 1-0 mbele ya Coastal Union na kumaliza nafasi ya tatu katika michuano hiyo ya kufungulia msimu, huku Yanga ikibebea Ngao na Azam ikimaliza ya pili. Wastani pia sio mbaya kwani ni 1-1 katika mechi mbili zenye ushindani mkubwa.


STRAIKA MPYA


Mara baada ya mechi dhidi ya Yanga zilianza kuenea tetesi kwamba, kocha Fadlu anataka aongezewe mshambuliaji mpya. Mshambuliaji atakayekuwa akiifungia timu hiyo mabao na kuipa uhakika wa kushinda mechi.


Tayari inaelezwa Simba iko katika hatua za mwisho ya kusajili straika wa kukidhi kiu ya Fadlu, baada ya kutoridhishwa na washambuliaji waliopo kwa sasa kikosini.


Simba ina Mashaka Valentino iliyemsajili kutoka Geita Gold, ina Steven Mukwala kutoka Asante Kotoko ya Ghana, pia ni wachezaji waliokuwapo msimu uliopita kama Freddy Michael na Kibu Denis, mbali viungo washambuliaji na mawinga wenye uwezo wa kutupia mipira nyavuni.


Ina Saleh Kabaraka, Ladack Chasambi, Edwin Balua waliokuwapo tangu msimu uliopita, huku ikiwa na sura mpya za Omary Omary, Jean Charles Ahoua na Joshua Mutale. Debora Mavambo na Augustine Okejepha licha ya kuwa viungo wa ukabaji lakini pia ni wazuri kwa kufunga mabao.


Lakini kocha kaona bado anahitaji mshambuliaji wa kumaliza kazi ya kucheka na nyavu na viongozi wametii agizo na sasa wapo sokoni. Lipo jina la Lionel Ateba, Mcameroon anayetokea USM Alger ya Algeria anayesemekana kupewa mkataba wa miaka miwili huku kipa Ayub Lakred ambaye ni majeruhi akihusishwa na mpango wa kuondolewa kwenye usajili ili kumpisha straika huyo.


TATIZO WALA SIO HILO


Inawezekana ni kweli kocha Fadlu anaona wachezaji hawampi kile anachokihitaji kwa sasa, lakini ukweli ni kwamba hajaliangalia tatizo la msingi la timu hiyo kwa hatua hii ya mapema.


Simba hii mpya ambayo haina hata miezi miwili haina tatizo la straika. Ina tatizo la kutengeneza nafasi zitakazowarahisishia kazi washambuliaji kufunga mabao ya kutosha.


Fadlu na wasaidizi wake ni lazima wapitie upya mechi zote ambazo timu hizo imecheza kuanzia kule kambini Ismailia, Misri hadi ya juzi ya kusaka mshindi wa tatu dhidi ya Coastal Unioni iliyotoka kufumuliwa mabao 5-2 na Azam katika mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii.


Kwa wanaokumbuka Simba ilicheza mechi tatu za kirafiki Misri, ikianza na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Canal SC, huku ikipata mabao kupitia kwa Ahoua aliyefunga mawili na jingine la Okejepha.


Ikacheza mechi nyingine mbili dhidi ya Telecom Egypt na Al Adalah ya Saudi Arabia na kushindi kwa mabao 2-1 kila moja, wafungaji wakiwa ni Valentino Mashaka na Ladack Chasambi walipowaua Telecom na Steve Mukwala na Joshua Mutale wakawazamisha Wasaudia.


Kwa mechi zile ni ngumu kutoa tathmini kwa kikosi kilivyocheza kwani mechi ilikuwa ni ya ndani, lakini timu iliporejea na kucheza katika Simba Day na kushinda mabao 2-0 yaliyofungwa na Debora Mavambo na Edwin Balua, kila mtu aliona.


Simba haikutengeneza nafasi nyingi tofauti na ilivyokuwa msimu uliopita ikiwa na wachezaji kama Saido Ntibazonkiza, Clatous Chama, Willy Onana, Babacar Sarr, Sadio Kanoute, Luis Miquissone na waliobaki kikosi cha sasa kama Kibu, Chasambi na Balua.


Bao la kwanza la Simba dhidi ya APR lililofungwa na Debora Fernandes, halikuwa la kutengeneza nafasi, kiungo huyo alitumia akili binafsi kwa kupiga shuti la kushtukiza kutokea mbali nje ya boksi mpira ukaenda wavuni na bao la pili lililofungwa na Balua, halikuwa la kutengeneza nafasi pia bali lilitokana na mpira wa kutengwa wa frii-kiki ya nje ya boksi iliyouvuka ukuta na kwenda moja kwa moja wavuni.


Dhidi ya Yanga, ilipolala kwa bao 1-0 timu haikutengeneza nafasi za kutosha, na ilipoiua Coastal Simba ilitengeneza nafasi moja ya maana iliyozaa bao lililofungwa Saleh Karabaka.


Kama timu haitengenezi nafasi, viungo hawawalishi washambuliaji, mabeki hawapigi krosi zinazowafikia kina Mukwala, ni lazima waonekane hawafai. Ni lazima Freddy na Mashaka waonekane uwanjani kama wakulima wanaokagua mashamba kwa kuzurura tu bila kuifungia timu mabao.


MUDA MFUPI MNO


Uamuzi wa Fadlu kutaka aletewe straika mpya kabla ya alionao kuwalisha mbinu na kuwakomalia kina Ahoua, Chasambi, Balua, Mutale na viungo washambuliaji wengine sambamba na mabeki wa pembeni kuwapa pasi na krosi zenye macho washambuliaji ni lawama ndani ya muda mfupi.


Wachezaji na hata kocha wana muda mfupi tangu waanze kuwa pamoja, hivyo kuwabebesha msala kina Mukwala ni kutaka kuwaonea tu, kwani hakuna pasi za kutosha za maana walizopewa eneo la lango la wapinzani kisha wakapoteza ili wapate kulaumiwa. Soka sio kama kukoroga chumvi katika mbona, ni mipango endelevu.


Hofu ni kwamba hata mshambuliaji mpya Msimbazi, iwe Ateba au yeyote atakayetua kabla dirisha la usajili halijafungwa leo usiku, kama hatalishwa mipira ataishia naye kulaumiwa tu kama Mukwala na wenzake.


Wanaomsaidia Fadlu ni lazima wamwambie ukweli kwamba Simba haitengenezi nafasi za mabao, kiasi cha kuona washambuliaji waliopo hawana uwezo wa kuibeba timu katika mashindano yaliyopo.


Timu ina muda mfupi tangu ijumuike pamoja na kufanya mazoezi kabla ya kucheza mechi hizo sita zilizopita ambazo huwezi kumhukumu mchezaji kama Mukwala aliyetoka Ghana akiwa na mabao ya kutosha. Ni ngumu kumsimanga Mashaka aliyetoka Geita akiwa kinara wa mabao, labda kama Fadlu amejishtukia kuwa Simba ni kubwa kuliko uwezo alionao na alivyoifikiria awali wakati akipewa kibarua angeweza kueleweka, kwani rekodi zinaonyesha kote alikofundisha alikuwa msaidizi tu na sio kocha mkuu.


Joto la kuwa kocha mkuu sasa ameanza kulihisi kwa klabu kubwa kama Simba ambayo mashabiki wake hawana uvumilivu, mambo yanaweza kumpalia mapema kuliko matarajio ya wengi. Angetuliza kichwa na kukomaliza kuwapa mbinu mawinga, viungo washambuliaji hasa Ahoua na mabeki wa pembeni kuwatengenezea nafasi nyingi washambuliaji ambao watajipanga katika eneo sahihi ili mambo yawe mepesi badala ya kuamini hawapati mabao kwa sababu ya kina Mukwala.


Ni lazima kocha Fadlu na wanasimba kwa ujumla kutoa muda zaidi ya wachezaji kuzoeana kwani ni wengi wao ni wapya na vijana wenye uwezo wa kushika maelekeo kwa ufanisi kadri muda utakapokuwa ukisonga mbele, pia wasijipe na ubora iliyonayo nayo Yanga, kwani watafeli mapema.


Yanga kwa misimu mitatu imezidi kuimarika na ina wachezaji waliozoeana kwa muda mrefu na wenye ubora tofauti na Simba mpya inayojengwa kwa sasa, ndio maana ni ngumu kumlinganisha Ahoua na maudambwidambwi aliyoondoka nayo Chama au wachezaji wengine waliopo Yanga. Simba ni timu nzuri inayojijenga kwa sasa, pia haina tatizo la mshambuliaji ila utengenezaji nafasi zitakazoweza kumalizwa na kina Mukwala katika nafasi sahihi. Hivyo tu, hayo mengine ni uzushi!

UTEUZI: Rais Samia Ateuwa Mawaziri, Ahamisha Viongozi

 

UTEUZI: Rais Samia Ateuwa Mawaziri, Ahamisha Viongozi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali huku akimteuwa Prof. Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria;


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, imeeleza kuwa William Lukuvi ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), huku Jenista Mhagama akiteuliwa kuwa Waziri wa Afya.


Kabla ya uteuzi huo, Mhagama alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) na Balozi Dkt. Pindi Chana yeye ameteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii.


Kabla ya uteuzi huo, Chana alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria, na sasa anachukua nafasi ya Angellah Jasmine Kairuki ambaye ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais.


Viongozi wengine walioteuliwa na kuhamishwa vituo vya kazi ni kama inavyoonekana katika viambatanishi.

UTEUZI: Rais Samia Ateuwa Mawaziri, Ahamisha Viongozi






Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...