Wednesday, July 24, 2024

MATOKEO ya Yanga Vs TS Galaxy Leo 24 July 2024

MATOKEO ya Yanga Vs TS Galaxy Leo 24 July 2024

MATOKEO ya Yanga Vs TS Galaxy Leo 24 July 2024

Klabu ya Yanga SC inashuka dimbani leo kuivaa TS Galaxy katika mechi ya pili ya michuano ya Kombe Kuu la Kimataifa la Mpumalanga inayofanyika Afrika Kusini.

Mchezo huo utafanyika kwenye uwanja kwenye uwanja wa Kanyamazane uliopo mji mdogo wa KaNyamazane katika jimbo la Mpumalanga.

Yanga ilipoteza mechi ya kwanza dhidi ya Augsburg ya Ujerumani kwa mabao 2-1 wakati TS Galaxy ilitoka sare ya mabao 2-2 na Mbabane Swallows ya Eswatini

Matokeo ya Yanga vs TS Galaxy

16:00 | YANGA 0:0 TS Galaxy

Simba Yatoa Neno Sakata la Aishi Manula, Kibu na Mwenda

 

Simba Yatoa Neno Sakata la Aishi Manula, Kibu na Mwenda

Klabu ya Simba imefunguka kuhusu wachezaji wao wawili, kipa Aishi Manula pamoja na beki wa pembeni, Israel Patrick Mwenda kutofika kambini nchini Misri mpaka sasa licha ya kuwa na mikataba na klabu hiyo.

Ahmed amesema hayo ikiwa ni wachezaji wanne sasa wa Simba ambao hawajafika kambini zikiwa zimepita wiki mbili tangu timu hiyo itue Ismailia kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya.

"Aishi Manula pamoja na Israel Mwenda wote bado hawajajiunga na kambi lakini hao wote sina majibu ya moja kwa moja kwamba ni kitu gani kinawafanya wasijunge na kambi, nitakapopewa taarifa rasmi nitawapa taarifa Watanzania nini kinaendelea juu yao.

"Hakuna changamoto hata kidogo, tuko imara na madhubuti mno, wachezaji wote ambao hawajawasili kambini mpaka sasa hawatuathiri hata kidogo, maandalizi yetu tunayoyafanya yamekamilika kwa asilimia zaidi ya 100.

"Hawa wachezaji ambao hawapo kambini kutokuwepo kwao hakutuathiri hata kidogo, ni kama kachumbari tu kwenye pilau. Wachezaji 29 wapo kambini nchini Misri, ni vikosi viwili kamili na unapata wachezaji wa akiba kwa hiyo tuko madhubuti," amesema Ahmed.

Wachezaji wa Simba ambao hawajafika kambini mpaka sasa ni;

Israel Mwenda (Hajatoa taarifa)

Aishi Manula (Hajatoa taarifa)

Kibu Denis (Mgomo baridi)

Aubin Kramo (Anatafutiwa timu kwa mkopo)

Lameck Lawi (Usajili wake una sintofahamu ambapo TFF imezitaka Simba na Coastal Union kumalizana kwa busara).

TFF Wafunguka Kuhusu Manara Kumaliza Adhabu yake ya Miaka Miwili



So


Saa chache baada ya Msemaji wa Yanga Haji Manara kutangaza kurejea katika majukumu aliyokuwa anafanya awali Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetoa baraka zote.

Manara jana alitangaza kurejea kazini baada ya kumaliza adhabu ya kufungiwa kwa miaka miwili iliyotolewa na Kamati ya Maadili ya TFF kupitia Ofisa Habari Clifforf Ndimbo amesema Manara yuko huru kuendelea na majukumu yake baada ya kukamilika kwa adhabu.

Ndimbo amesema mbali na Manara kumaliza adhabu pia amelipa kiasi cha sh 10 Milioni ikiwa ni faini iliyoambatana na kifungo hicho.

"Manara yuko huru kweli na hata huo mkutano alioufanya hajakosea kitu kwa kuwa hajafanya kosa lolote kikanuni adhabu yake ilimalizika" amesema Ndimbo.

"Ukiachana kumalizika kwa adhabu hiyo kutokana kudaiwa kufanya makosa ya kimaadili alipowaruzana na Rais wa TFF Wallace Karia katika Fainali ya Kombe la FA kati ya Yanga dhidi ya Coastal UNion ya Tanga uliochezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid JIjini Arusha.

Source

Mati super brand's Ltd ndo mdhamini wa Fountain Gate Fc

Na John Walter -Babati 

Kampuni ya Mati Super Brands Limited inayozalisha vinywaji changamshi iliyopo mjini Babati Mkoani Manyara  imedhamini timu ya mpira wa miguu  inayoshiriki ligi kuu ya soka Tanzania bara ya Fountain Gate fc kupitia kinywaji chake kipya  cha Tanzanite Royal Gin ambapo timu hiyo imeingia makubaliano ya udhamini wa mwaka mmoja na kampuni hiyo .

Akizungumza katika Hafla ya kusaini mkataba wa udhamini huo,Mkurugenzi wa Kampuni ya Mati Super Brands Limited David Mulokozi amesema kuwa wameamua kudhamini timu hiyo ili kutoa fursa kwa wakazi wa Mkoa wa Manyara kupata burudani ya soka kutoka kwa timu ya Fountain Gate fc na kunufaika na  fursa za uwepo wa timu hiyo na timu mbalimbali zitakazofika mkoani hapa ikiwemo wafanyabiashara,wajasiriamali .

Mulokozi amesema kuwa uwepo wa timu hiyo utachochea maendeleo ya michezo mkoani Manyara Pamoja na maendeleo ya kiuchumi kutokana na timu hiyo kupiga kambi mkoani Manyara .

"Leo Tumewaletea Habari Njema kwa mkoa wa Manyara kuwa timu hii pendwa ya Fountain Gate imehamia Mkoani Manyara chini ya Udhamini wa Kampuni ya Mati Super Brands Limite kupitia kinywaji kipya cha Tanzanite Royal Gin" Anaeleza David Mulokozi Mkurugenzi wa Kampuni ya Mati Super Brands Limited.

Mkurugenzi wa Timu ya Fountain Gate Japhet Makau ameishukuru Kampuni ya Mati Super Brands Limited kwa udhamini mnono na kuahidi kufanya vizuri katika mashindano mbali mbali ya kitaifa na kimataifa.

Afisa Mtendaji Mkuu  Timu ya Fountain gate kidawawa Thabita amesema wachezaji wote wana hali nzuri na wako tayari kushiriki mashindano wakati wowote na kuongeza kuwa udhamini huo utaongeza ufanisi mkubwa kwenye timu hiyo.

Tuesday, July 23, 2024

Harmonize: Nikiacha Muziki, Nitakuwa Daktari

 

Harmonize: Nikiacha Muziki, Nitakuwa Daktari


MSANII Rajab Kahali, maarufu kwa jina la Harmonize, mmiliki wa Kundi la Konde Music kwa mara ya kwanza ameeleza ndoto yake ya kile anachopanga kukifanya baada ya kustaafu kazi yake ya muziki.


Katika mahojiano, msanii huyo alieleza kuwa anafahamu kabisa kuwa hatakuwepo kwenye tasnia ya muziki milele na tayari amebainisha ni kitu gani ataridhika nacho pindi taaluma yake ya muziki itakaposhuka.


Harmonize ambaye alisherehekea miaka yake 30 miezi michache iliyopita, alifichua ndoto yake ya kuwa daktari ili kuokoa maisha. Alieleza nia yake ya kusomea udaktari baada ya kustaafu muziki akiwa na miaka 45 hadi 50.


"Nimewaza huko mbeleni kazi yangu ya muziki ikishuka labda nikiwa na umri wa miaka 45-50 nitafikiria kusomea udaktari, angalau mwaka mzima ningependa kufanya kazi hospitalini ili kusaidia watu," Harmonize alisema.


Msanii huyo alieleza kuwa mbali na lengo lake la kutoa misaada ya kibinadamu kwa kuwatibu wagonjwa, pia anataka kuona furaha kwenye nyuso za watu kutokana na fani hii anayofikiria kuifanya licha ya kuishia darasa la saba.

KAPINGA: Taasisi zinazotoa huduma za kijamii kuunganishwa Umeme


Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema kuwa Taasisi zote zinazotoa huduma za kijamii kama shule na vituo vya afya pamoja na nyumba za ibada zitafikishiwa umeme.

Naibu Waziri Kapinga ameyasema hayo  Julai 22, 2024 wakati akiwasha umeme katika Shule ya Sekondari Nyasa iliyoko katika Kijiji cha Chimate wilayani Nyasa, Mkoa wa Ruvuma. 


"Sisi kama Wizara ya Nishati ni kuhakikisha tunaongeza tija katika taasisi hizi zinazotoa huduma kwa kufikisha umeme. Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan anahangaika usiku na mchana kutafuta fedha za kuboresha maisha ya Watanzania kila siku na kazi yetu kubwa ni kuhakikisha taasisi na maeneo yote yenye umuhimu yanafikiwa na umeme"amesema.

Aidha amesema Shirika la Umeme nchini (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wamejidhatiti katika maeneo ambayo kuna taasisi za kijamii kama shule, vituo vya afya, makanisa na misikiti kwa kuhakikisha vinafikiwa na umeme ili kuboresha huduma za kijamii katika Taifa letu," amesema Kapinga.


Awali akitoa taarifa ya utekelezaji Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa REA, Eng. Robert Dulle amesema kuwa gharama za kufikisha umeme katika kijiji hicho ni shilingi Milioni 286.

Eng. Dulle ameongeza kuwa Mkoa wa Ruvuma unajumla ya Vijiji 554 na mpaka kufikia Julai 2024, vijiji 542 sawa na asilimia 97.8 vimepata huduma ya umeme kupitia miradi inayotekelezwa na REA huku akihamasisha wananchin kuchangamkia fursa za uwepo wa umeme vijijini kufanya shughuli za kiuchumi zitakazoboresha maisha yao.

Kwa upande wake, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Nyasa, Mwalimu John Ndelwa ameipongeza REA kwa kufikisha umeme shuleni hapo na kuahidi kuwa watatumia fursa ya umeme huo kuwafundisha wanafunzi masomo ya jioni na hivyo kuongeza ufaulu.

Ameongeza kuwa uwepo wa umeme utawawezesha kuwa na mitihani mingi ya majaribio kwa kuwa watakuwa na uwezo wa kuchapa mitihani wenyewe shuleni tofauti na awali ambapo walikuwa wanalazimika kutumia gharama kubwa kwenda kuchapisha katika steshenari.
 
Imeandikwa na Daudi Manongi na Iddi Mwema-Nyasa

Monday, July 22, 2024

Simba Kiboko, Yamfunga Mtu bao 3 Bila Pre Season




Mechi ya dakika 120 imekamilika huko Misri na Simba kufanikiwa kushinda jumla ya magoli 3-0 dhidi ya El Qanah katika mchezo wa kirafiki wa mwendelezo wa maandalizi ya msimu mpya.

Mchezo huo umechezwa kwa vipindi vitatu tofauti ambapo kila kipindi kilikuwa na dakika 40.

Magoli ya Simba yamefungwa na Ahoua ameingia kimiani mara mbili na Okejepha

USIPIME: Vikosi vya Yanga na Simba ni vya Moto Hatari, Cheche Zitalipuka Msimu Ujao

 

USIPIME: Vikosi vya Yanga na Simba ni vya Moto Hatari, Cheche Zitalipuka Msimu Ujao

Simba na Yanga ni timu zilizokamilisha usajili wa idadi ya nyota 12 wa kigeni, Wekundu wakinasa mastaa saba wapya wanaoungana na watano waliosalia kutoka kikosi cha msimu uliopita, wakati Wananchi wameongeza silaha tano mpya zinazoungana na wengine saba waliosalia kikosi kilichopita.

Katika dirisha la usajili lililo wazi kwa sasa hadi Agosti 15, imeshusha mabeki wawili akiwamo wa kushoto, Valentin Nouma na yule wa kati, Chamou Karabou, viungo Charles Ahoua, Debora Mavambo, Augustine Okejepha pamoja na washambuliaji  Joshua Mutale na Steven Mukwala.

Nyota hao wanaungana na kipa Ayoub Lakred, beki Che Fondoh Malone, kiungo Fabrice Ngoma na washambuliaji Willy Onana na Freddy Michael.

Hivyo kama kocha Fadlu ataamua kuanza na kikosi kitupu cha wageni basi atamkosa beki wa kulia tu, lakini mziki mzima utakuwa umekamilika kwa kuanza na Ayoub aliyeongeza mkataba wa mwaka mmoja, huku kushoto akiwa na Nouma na mabeki wa kati watasimama Che Malone na Karabou.

Eneo la kiungo Simba itaweza kuanza na Ngoma akisaidiwa na nyota watatu wapya Debora, Okejepha na Joshua Mutale, wakati safu ya ushambuliaji itakuwa chini ya Jean Ahoua na Steven Mukwala wakati Freddy ataanzia benchi kabla ya kuingizwa baadae kuliamsha.

Kwa Yanga, inayoshikilia mataji ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho kwa misimu mitatu mfululizo, imesajili beki Chadrack Boka,viungo Clatous Chama aliyekuwa Simba na Duke Abuya aliyekuwa Singida BS, huku eneo la ushambuliaji kukiwa na Prince Dube kutoka Azam FC na Jean Baleke aliyewahi kuwika na Simba.

Nyota hao wanaounga na kipa Diarra Djigui, Yao Kouassi, Khalid Aucho, Pacome Zouzoua, Maxi Nzengeli, Stephane Aziz KI na Kennedy Musonda waliokuwapo msimu uliopita, hivyo kama Gamondi ataka kujibu mapigo ya Fadlu ya kushuka na nyota wa kigeni watupu, basi ni eneo la beki ya kati ndio atakuwa na mapengo kwani haitakuwa na namba nne wala tano, baada ya Gift Fred kutemwa kikosini.

Langoni Yanga itaanza kama kawaida na kipa namba moja, Djigui Diarra, beki wa kulia akiwa ni Yao, huku kushoto akisimama Boka, lakini italazimika kuwaingiza Bakar Mwamnyeto, Dickson Job au Ibrahim Bacca, kucheza beki ya kati.

Kwa eneo la kiungo Gamondi ana mashine za maana kama Aucho, Maxi, Pacome, Chama na Abuya, japo atalazimika mmoja kumuanzisha benchi ili kupata uwiano mzuri, huku katika eneo la mbele la ushambuliaji anaweza kumtumia Aziz KI na Dube, huku Baleke na Musonda kuanzia benchi au kinyume chake, kwani katika eneo hilo kama ilkivyo kwa kiungo kumejaa mafundi watupu wa kumrahisishia mambo.

CHAMA LA WAZAWA KWA KILA TIMU

Hapa sio Yanga wala Simba wote wamekamilika na hakuna haja ya makocha kuahangika kama ilivyokuwa kwa vikosi vya nyota wa kigeni watupu. Tuanze na Yanga, hapa Gamondi anaweza kuanza na Abubakar Khomeiny au Aboutwalib Mshery, huku beki wa kulia akisimama Kibwana Shomari na kushoto kuna Nickson Kibabage wakati mabeki wa kati anaweza kumgtumia Job na Bacca, huku Mwamnyeto akasubiri.

Viungo atakuwa na machaguo yua kutosha kwani ana Jonas Mkude, Mudathir Yahya, Denis Nkane ambaye huenda hapa atapata nafasi baada ya kusugua sana benchi na Salum Abubakar 'Sure Boy', huku Aziz Andambwile akisubiri nje wakati washambuliaji watakuwa ni Clement Mzize na Farid Mussa.

Kwa upande wa Simba huko ndiko kuna balaa zaidi, kwani Kocha Fadlu anaweza kuanza langoni na Ally Salim au Hussein Abel, wakati beki wa kulia akiwa Shomary Kapombe, Kelvin Kijiri au David Kameta 'Duchu', huku kushoto kuna nahodha Mohamed Hussein 'Tshabalala na kati wakiwa Abdulrazack Hamza na Hussein Kazi.

Safu ya kiungo itakuwa chini ya Yusuph Kagoma, Mzamiru Yassin, Ladack Chasambi, Awesu Awesu huku Omary Omary akisubiri nje na kule mbele wataanza Kibu Denis na Edwin Balua na Valentino Mashaka itabidi asubiri benchi ama kinyume chake kwani wote wanaonekana ni moto mkali.

KAMA WAKIHITAJI MSETO NI  BALAA

Kama makocha wote wawili wataona jahu kuanza na vikosi vya wachezaji wa sampuli moja, basi hapa watafanya mseto wa maana unaozalisha kikiosi kikali zaidi na balaa ndipo linaweza kutokea kama inavyokuwa siku zote zinapokutana timu hizi za Kariakoo zilizotawala soka la Tanzania Afrika Mashariki.

Timu zote zinaweza kuwa na vikosi vizito zaidi endapo zitachanganya wazawa na wale wa kigeni na kila moja ikawa na mziki mzito utakaosumbua ndani na nje na hapo Kwa Mkapa siku ya Nane Nane moto utawaka kwelikweli, kwani zote sasa zinaweza sasa kupangwa bila tatizo kuanzia langoni hadi mbele.

Yanga ya Gamondi inaweza kuanza na mziki huu, Diarra, Yao, Kibabage, Bacca na Job kama ambavyo walianza juzi dhidi ya FC Augsburg, huku eneo la kiungo akasimama Aucho, Andambwile,Mudathir au hata Mkude wawili kati ya hao, kisha juu yao akacheza Chama, Maxi wakati mbele kukiwa na Aziz Ki na Baleke au Dube. Usisahau benchi kutakuwa na mashine nyingine za maaana kama Pacome, Mzize, Musonda na Abuya.

Kwa upande wa Simba sasa hapo Fadlu atalipanga jeshi kwa kikosi kitakachoundwa na Ayoub, Kapombe, Tshabalala, Che Malone, Karaboue, huku viungo wakiwa Ngoma, Kagoma, Mutale na Okejepha wakati eneo la mbele litakuwa na Mukwala na Ahoua.

Mashine nyingine kama Freddy, Kibu, Balua, Chasambi na wengine zitasikilizia pale watakapoiunuliwa ili kwenda kuwapokea wenzao.

NIDA YAWATAKA WENYE VITAMBULISHO VILIVYOFUTIKA KUVIREJESHA

Mwananchi akichukuliwa alama za vidole katika moja ya ofisi za NIDA kwa ajili ya Utambulisho wake wa Taifa.

MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imewataka wananchi wote ambao vitambulisho vyao vimepata hitilafu ya kufutika maandishi kuvirejesha katika ofisi za NIDA ama katika ofisi za Serikali za Mitaa, Kata, Vijiji na Shehia ambako vitakusanywa na kurejeshwa kwa ajili ya kuchapishwa upya bila malipo yeyote kwa mwananchi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Idara ya Vitambulisho kutoka NIDA Edson Guyai wamepokea taarifa ya kuwepo kwa Vitambulisho vichache kufutika taarifa zailizochapwa mbele au nyuma ya kitambulisho mfano majina, picha au Namba ya Kitambulisho au tarehe ya kuzaliwa.

Mkurugenzi huyo amesema takwimu za Mamlaka hiyo zinaonyesha kuwa vitambulisho vyenye hitilafu hiyo ni 21,224 sawa na asilimia 0.09 ya vitambulisho 21, 32,098 viliyozalishwa.

Ametoa rai kwa mwananchi ambaye Kitambulisho chake kitakuwa na changamoto hiyo akirudishe ofisi ya NIDA au kwa mtendaji alipokichukua ili virudishwe na kuchapishwa upya.

Amesema kumekuwa na upotoshaji kuhusu ubora wa vitambulisho vya Taifa kutokana na changamoto hiyo ndogo iliyojitokeza na amesisitiza kwamba Vitambulisho vya Taifa vinavyotolewa na Mamlaka hiyo vina ubora unakidhi viwango vya kimataifa.

Amedokeza kuwa kwa sasa wataalamu wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha tatizo hilo kama ni mashine, wino au kadi. Hii itawezesha kufidiwa kwa kadi hizo kama yalivyo matakwa ya mkataba bila Serikali kuingia gharama yeyote.

Mkurugenzi huyo amesema hitilafu ndogondogo ni jambo la kawaida kutokea katika sekta ya uzalisha wa bidhaa duniani huku akieleza kuwa hata kammpuni kubwa za uzalishaji kama magari na simu za mkononi hupata changamoto kama hizi.
Mwananchi akipigwa picha kwa ajili ya utambulisho wa Taifa.
Mwananchi akikabdhiwa Kitambulisho chake katika moja ya ofisi za Serikali ya Mtaa
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...