Friday, July 30, 2021

PICHA :Rais Samia alivyoipokea Ndege mpya Airport DSM





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo July 30, 2021 amepokea ndege mpya aina ya Bombadier Dash 8 – Q400 katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 1 Jijini Dar es Salaam.


Millardayo.com imekusogezea picha 13 ushuhudie tukio hilo lilivyokuwa Airport DSM pamoja na muonekano wa ndege hiyo mpya



Huyu Hapa Aliyekuwa Waziri wa Tanzania Ambae Alijivua Uwaziri na Kujiunga na Jeshi Kwenda Vitani Kumpiga Iddi Amini



Marehemu Major Gen. Muhiddin Kimario, mmoja ya mawaziri wawili tu wa Mambo ya Ndani katika historia ya Tanzania kuwahi kudumu katika nafasi hiyo kwa zaidi ya miaka 5.

Alitumwa na Mwl Nyerere kuwaaga wanajeshi kwenda kumng'oa Nduli Idd Amin, akiwa anahutubia katika uwanja wa Nyamagana ghafla akajivua Uwaziri na yeye akaenda vitani.

" Mkuu wa mkoa naomba ufikishe taarifa hii kwa Mh Rais kwamba najivua Uwaziri na naamuwa kurudi Jeshini kuungana na wenzangu leo kwenda kumshikisha Adabu Amin"

Tanzia: Babu wa Loliondo Afariki Dunia



Ambilikile Mwasapile maarufu kama Babu wa Loliondo amefariki dunia akipatiwa matibabu Hospitali ya Digodigo

Babu wa Loliondo inadaiwa aliugua muda mrefu na akawa akijitibu kwa miti shamba, alipoenda hospitali leo saa sita alikuwa amechelewa, akafariki saa nane

Babu wa Loliondo alipata umaarufu kwa dawa yake aliyodai inatibu magonjwa yote

Wiki ya AZAKI 2021 kufanyika Jijini Dodoma, Wadau wakutana kufanya uzinduzi rasmi Dar

 


MSAJILI wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGOs) Vickness Mayao amezindua rasmi Wiki ya AZAKI inayotarajiwa kufanyika Oktoba 25 hadi Oktoba 29 mwaka huu huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza viongozi wapya wa Baraza la Kitaifa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali kupitia Mwenyekiti na timu yake yote.

Akizungumza leo Julai 29,2021 jijini Dar es Salaam wakati akizindua wiki hiyo ya AZAKI,Mayao amesema hiyo ni mara yake ya pili sasa kupata nafasi ya kukutana na wakuregenzi wa Asasi za kiraia nchini pamoja na wadau wengine wa maendeleo, baada ya mkutano wa kikao kazi uliofanyika Januari mwaka huu. 


"Ama kwa hakika fursa hizi za kukutana nanyi zimeendelea kuwezesha  uimarikaji wa mahusiano na mashirikiano kati ya asasi za kiraia na Serikali kupitia Ofisi ya Msajili na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini. Nichukue nafasi hii kutoa pongezi za dhati kwa mara nyingine tena kwa uongozi mpya wa Baraza la Kitaifa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali, kupitia Mwenyekiti na timu yake yote. 

"Wizara Pamoja na ofisi yangu tulipata faraja kubwa kuona kuwa sasa uongozi na uratibu wa sekta ya asasi za kiraia nchini umerejea mahali pake. Sote ni mashahidi wa madhara yaliyojitokeza kutokana na ukosefu wa uongozi na uratibu wa sekta ya asasi za kiraia nchini kwa miaka kadhaa.Nipende kuwaahidi kuwa ofisini yangu iko tayari kushirikiana nanyi kwa karibu sana kuhakikisha ustawi na usimamizi dhabiti wa sekta ya asasi za kiraia nchini,"amesema.

Aidha ametoa pongezi kwa Kamati ya uchaguzi wa NaCoNGO chini ya Mwenyekiti wake Flaviana Charles wakili msomi na uratibu makini wa mchakato mzima kupitia Mkurugenzi wa Foundation for Civil Society Francis Kiwanga."Hakika mmedhihirisha bayana nguvu ya umoja na mshikamano ambayo ikiendelea kutumika vizuri itapelekea mapinduzi na maendeleo ya hali ya juu kwa sekta hii ya Asasi za kiraia nchini." 

Kuhusu Wiki ya AZAKI , Mayao amefafanua wamekutana kwa ajili ya tukio muhimu kwa wadau wa maendeleo nchini ikiwemo Asasi za kiraia, sekta binafsi, pamoja na Serikali ambayo ndio mdau mkubwa wa maendeleo katika taifa letu. "Sote ni mashahidi  wa umuhimu na matokeo chanya ya Wiki ya  AZAKI toka uzinduzi wake  mwaka wa 2018, ikiwemo kuongezeka kwa umoja na mshikamano miongoni mwa wadau wa maendeleo. 

"Kuimarika kwa mshikamano kati ya Asasi za kitaifa na za ngazi ya jamii/mashinani, asasi za wazawa na mashirika ya Kimataifa, wakala wa sekta binafsi pamoja na taasisi za serikali na vyombo vya maamuzi.Tunashuhudia pia kuimarika kwa ushiriki wa Asasi katika masuala ya kisera kwa kujiamini zaidi na kwa kushirikiana na vyombo vya serikali pamoja na Bunge katika misingi ya kuaminiana,"amesema.

Aidha kupitia Wiki ya AZAKI, wameona kuongezeka kwa ushirikishanaji taarifa na upashanaji habari miongoni mwa wadau wa maendeleo. Pia kuongezeka kwa uelewa miongoni mwa  Jamii ya Watanzania kuhusu  kazi na huduma zitolewazo na Asasi za kiraia na wadau wa maendeleo, sambamba na mchango wao katika ujenzi wa Taifa.

"Kwa miaka miwili mfululizo 2018 na 2019, Wiki ya AZAKI ilifanyika Jijini Dodoma na kuwaleta kwa pamoja wadau muhimu wa  maendeleo.  Zaidi ya Asasi 1,000 kutoka mikoa yote nchini zimeshiriki katika jukwaa hili tena kwa kujigharamia ushiriki wao katika warsha na maonesho ya kazi za Asasi za kiraia.Kauli mbiu ya Wiki ya AZAKI kwa mwaka 2018 ilikua "Kuelekea Uchumi wa Viwanda: Watu, Sera na Utekelezaji". Ambapo kwa mwaka 2019 kauli mbiu ilikua "Ubia kwa Maendeleo: Ushirikiano kama Nguzo ya Maendeleo nchini Tanzania.

Ameongeza kauli mbiu ya mwaka huu ni mchango wa sekta ya Asasi za kiraia katika maendeleo ya nchi, kwa ufupi AZAKI na maendeleo huku akisisitiza  Wiki hiyo ya AZAKI inatarajiwa kufanyika mwezi wa Oktoba 25 - 29 Jijini Dodoma, ikitanguliwa na maonesho ya kazi za Asasi za kiraia nchini Oktoba 23 na Oktoba 24 mwaka huu.

Amesema Wiki ya AZAKI ya mwaka 2018 ilileta mwamko mkubwa miongoni mwa wadau wa sekta kuonesha na kuudhihirishia umma wa watanzania mchango wa AZAKI katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini. Miongoni mwa jitihada zilizochukuliwa ni kutoa ripoti ndogo ya  mchango wa AZAKI katika uchumi wa Taifa. 

"Niwahakikishie kuwa ofisi yangu, kwa kushirikiana na NaCoNGO pamoja na wadau wa kamati ya maandalizi itahakikisha ripoti hii inakamilika kwa wakati na kuwasilishwa   katika wiki ya AZAKI mwezi Oktoba mwaka huu 2021,"amesema.

Aidha amesema toka kuanzishwa kwa Wiki ya AZAKI Ofisi ya Msajili imekuwa ikishiriki kikamilifu katika maandalizi na utekelezaji wa shughuli hii muhimu, kama mshauri mkuu kwa kamati ya maadalizi. "Mwito wangu kwa kamati ya maandalizi  ni kuendelea kuboresha ushirikiano wao kuhakikisha AZAKI zinakua imara na zinaleta mchango unaostahili katika maendeleo ya nchi". 

Kwa upande wake Mwenyekti wa Bodi wa Baraza la Uratibu wa NGOs Taifa Lilian Badi amesema ni mara yake ya kwanza kukutana na wadau hao tangu yeye na wenzake 29 wachaguliwe kutoka mikoa 26 na wawakilishi wanne wa makundi maalum kuwa wajumbe wa baraza la uratibu wa NGOs Tanzania.

Aidha amesema ni muhimu kutambua kwa miaka mingi sasa Foundation for Civil Society imekuwa kinara katika kuzijengea uwezo NGOs kupitia ruzuku na hata kuwapatia mafunzo mbalimbali na kuwaunganisha kwa njia kadhaa."Na leo hii tunapozindua wiki ya AZAKI ni ushahidi tosha kuhusu ufanisi na dhamira yetu ambayo haijawahi kupwata na tunajua tukio hili mmekuwa mkilifanya kila mwaka."

Ametumia nafasi hiyo kutoa mwito kwa Foundation for Civil Society na wadau wengine waendelee kuunga mkono chombo hicho muhimu kilichoundwa kisheria kwa kuhakikisha sio tu kinafanya kazi zake kwa ufanisi bali NGOs zinaelewa majukumu na nafasi ya NaCoNGO kisheria na kiuendaji ili kuepuka chombo hicho kujikuta kwenye migogoro ya mara kwa mara na isiyo na tija au kudhoofika.

Awali Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) anayewakilisha Asasi za kiraia amesema ameshauri vitu vya tatu, cha kwanza wakati umefika fedha za ufadhili ambazo zinakuja kwa ajili ya ASASI za kiraia zitekeleze mipango iliyopo kwani takwimu zinaonesha fedha hizo zinapoingia ni asilimia moja tu ndio inakwenda kwenye NGOS za ndani na iliyobakia inakwenda kwenye mashirika ya kimataifa, hivyo umefika wakati ASASI za kiraia nchini kushiriki kikamilifu kwenye maendeleo.

Amesema eneo la pili ambalo ameshauri ,amesema sekta ya AZAKI mara nyingi inahesabiwa kama sehemu ya sekta binafsi, lakini sekta binafsi ni tofauti ambayo inawafanyabishara zaidi na anapokwenda kuongea mwakilishi wa seta binafsi hawezi kuwa anawakilisha sekta ya AZAKI, hivyo ni vema AZAKI nao wakatambula na mwisho amesema bado kunachangamoto katika kufanya kazi wao kama sekta hasa katika kutekeleza matakwa ya kisheria hasa sheria za kodi.

"Kuna mkanganyiko mkubwa kwa mfano unakuta mimi ni mkurugnzi natumia vijana wanaojitolea lakini unapowalipa posho TRA anahesabu wale kama wafanyakazi kitu ambacho sio sahihi, kwa hiyo bado kuna mkanganyiko wa uelewa wetu katika sheria ya kodi kwa mashirika ambayo sio ya kiserikali na hiyo inachangia sisi kukwama."

Serikali itahakikisha zao la mkonge linaimarika - RC Malima

SERIKALI Mkoani Tanga imesema itahakikisha zao la Mkonge linaimarika kutokana na ongezeko la mahitaji ya bidhaa zitokanazo na zao hilo duniani yanayolenga kuachana na matumizi ya bidhaa za Plastiki ambazo zina athari kwa Jamii. 

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima wakati wa ziara yake ya kukagua ukarabati wa Mashine za kuchakata mkonge ambapo awali zilikua chakavu hali iliyokua ikisababisha kushuka kwa uzalishaji wa zao la Mkonge. 

Mkuu huyo wa mkoa alisema kwa miaka mingi nguzo ya uchumi ya Mkoa huo ilikuwa zao la Katani na miaka 50 iliyopita Tanga ilikuwa inazalisha tani 150,000 lakini baada ya marekebisho na nguvu kubwa mkoa wa Tanga inazalisha tani 35000.

Alisema hivi sasa Serikali ya Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu imeweka mkakati wa makusudi wa kuzalisha zao la Mkonge Kitaifa kutoka Tani 35,000 hadi kufikia Tani 120,000.

Aidha alisema mkakati huo unasimamiwa na Waziri Mkuu Kasim Majaliwa ambao wakuu wa mikoa na wadau wengine wote wamekuwa ni sehemu ya mpango huo mafanikio yake yapo hapa wilayani Korogwe.

Alisema ili kufikia Tani 100,000 za Mkonge wanaweza kufikia huko kwa kushirikiana na wawekezaji wakubwa wakiwemo Mohamed Interprises Limited, Amboni Platation, Kwale, Palet.

Mkuu huyo wa mkoa aliekeza lakini bodi inajua na ina maelekezo ya Waziri Mkuu na Serikali juu ya mkakati huo maana yake wanataka kuwa na uzalishaji wa mkonge mkulima ashiriki kama mmiliki wa uzalishaji huo na sio kama manamba na namna ya kufanya hivyo ni kupitia kwa vyama vya ushirika Amcos kama serikali, Mrajis wa vyama wataanza kuwa na uwezo wa uongozi na rasimali ili iweze kuwa na uzalishaji mkubwa zaidi.

Alisema vyama vya Ushirika (AMCOS) wana ubia katika uzalishaji na Kampuni ya Sisalana ambayo inamilikiwa na Shirika la

Hifadhi za Jamii (NSSF) hivyo Sisisala lazima ijengewe uwezo wa kupokea  zao linalotoka kwa Mkulima kutokana na kwamba hivi sasa Sisalana wanapokea Tani 6000 kwenye Amcos zote na wana uwezo wa kupokea tani 11000 .

Aliseam hivyo yeye amefika na timu yake kuweza kutengeneza mkakati ili hizo tani 11000 ziwafikie Sisalana na zipate kuchakatwa na mkulima aweze kupata haki yake pamoja licha ya kwamba huko kuna changamoto za pande zote mbili za Amcos na Sisalana na nyengine ambazo lazima utatuzi wake upatikana kwa Serikali ikiwemo suala la miundombinu inayopitisha


Awali akizungumza Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini kutoka Mfuko wa Taifa wa Hifadhi za Jamii (NSSF) Balozi Alli Siwa alisema sheria ya kuanzishwa kwa mfuko huo inawaruhusu kuingia kwenye uwekezaji ndio maana wameshiriki kwenye ziara ya Mkuu wa Mkoa kwenye Corona ambazo zinamilikiwa na Kampuni ya SISALANA ambayo ni kampuni tanzu ya NSSF.

Alisema kampuni hiyo imepewa dhamana ya kuendesha Corona tano kwa madhumuni ya kuweza kurejesha fedha za wanachama ambapo wanaendesha shughuli za biashara hiyo kwa kushirikiana na Amcos kazi yao kubwa ni kuchakata majani ya katani ili Amcos ziweze kuuza brashi ambayo inaitwa Singa na wao wanaweza kupata tozo kwa ajili ya kuchakata.

Alisema hilo limewapelekea kwenye biashara ya mkonge na kwao hiyo haitoshi kuchakata kutokana na kwamba itawachelewesha kurudisha fedha zao wanazotaka kuzipata na pili wanataka biashara hiyo iwe na maana katika kutunishia mfuko wa Pensheni ili waweze kuwa na uwezo mkubwa wa kulipa pensheni kila inapohitajika kwa wanachama wao.


Naye kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Sisalana Elizaberth Kalambo alisema walianza kazi yao kwa kufanya ukarabati katika mitambo katika kiwanda cha Usambara na baada ya hapo watahamia Mwelya ili kuhakikisha mitambo inakuwa katika hali nzuri.

Alisema wakati wanafanya ukarabati na matengenezo kwenye mitambo hivyo wanaomba wakulima wa mkonge wanaosimamiwa na Amcos tano za Mwelya, Magoma, Hale, Ngombezi na Magunga wanaomba wakulima wawape ushirikiano ili waweze kufanya maboresho.

Alisema kwa sababu wanapofanya matengenezo makubwa wanasimamisha uzalishaji kwa muda wa usipoungua wiki mbili mpaka tatau hivyo wanasisitiza kwa wakulima waongeze kasi ya upelekaji wa majani kwa kupeleka awamu mbili ili kuepuka hasara watakazokutana nazo wakati wanaposimamisha uzalishaji kwa siku hizo.

 


Source

Wayne Rooney Aomba Radhi Baada ya Picha zake Akiwa na Wasichana Walio nusu Uchi Kuvuja



Mchezaji wa zamani wa Uingereza na Manchester United, Wayne Rooney ameomba radhi kwa familia, mke wake Coleen klabu ya Derby County na jamii kwa ujumla kufuatia kusambaa kwenye mitandao ya kijamii picha zake ambazo zinamuuonesha akiwa hotelini amelala kwenye kiti huku akizungukwa na wasichana watatu wengine wakiwa na nguo ya ndani pekee.



Rooney ambaye ni baba wa watoto wanne na mke wake Coleen (35) aliamua kulipeleka mbele sakata hilo, huku akiwalipa wasichana hao paundi milioni 1 akinunua haki miliki ya picha hizo baada ya kuwatuhumu kwa kumsaliti na kuwataka wamuombe msamaha.

Akizungumza na Sky Sports News baada ya mchezo wa kirafiki baina ya Derby dhidi ya Real Betis siku ya Jumatano, Rooney amesema alifanya makosa.

Model Tayler Ryan pictured with ex-England football ace Rooney while they were partying in Manchester on Saturday night

"Nilikwenda kwenye 'private party' nikiwa na marafiki zangu wawili, ningependa kuomba radhi kwa familia yangu na klabu kwa picha zilizokuwa zikisambaa."

"Ninafuraha kwa Derby County kunipatia nafasi hii kuirudisha klabu hii kule ilikokuwa awali, nitafanya kila lililondaniya uwezo wangu kuhakikisha nafanikkisha hilo."

Imeandikwa na Hamza Fumo Instagram @fumo255


MWANAMKE AFARIKI KWA KUUNGUA MOTO GESTI


Kamanda wa Polisi mkoani Kagera Revocatus Malimi
***
Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Neema Bayo anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 40 hadi 49 mwenyeji wa Babati mkoani Arusha, amepoteza maisha na wengine wanne kunusurika kifo, baada ya nyumba ya kulala wageni walimokuwa wamelala kuteketea kwa moto.

Moto huo ulitokea usiku wa kuamkia Julai 29 mwaka huu, katika nyumba ya kulala wageni ya New Anti, eneo la Muleba mjini wilaya ya Muleba mkoani Kagera, umeteketeza jengo lote na vitu vyote vilivyokuwa ndani.

Akizungumzia eneo la tukio Kamanda wa Polisi mkoani Kagera Revocatus Malimi amesema wakati moto ukitokea katika nyumba hiyo kulikuwa na watu watano wakiwamo wageni watatu, mhudumu na mtoto wa mhudumu huyo.

Kwa upande wake Afisa Uhusiano wa Shirika la Umeme nchini TANESCO wilaya ya Muleba, Sadam Kaijage amesema kuwa walipokea taarifa kwa simu na kuwahi eneo la tukio ili kudhibiti moto huo usienee zaidi, na kwamba uchunguzi umeanza ili kubaini chanzo cha moto huo.

Naye mhudumu wa hoteli hiyo iliyoteketea kwa moto Farida Mwise amesema kuwa umeme ulikatika saa nne usiku na wakati wanalala hakukuwa na umeme, na alipoamka usiku kumpa mtoto wake uji kabla hajasinzia alisikia kishindo ndipo alipofuatilia akagundua kuwa nyumba inaungua, akakimbia kuwaamsha wateja na kisha kukimbilia nje akiwa amembeba mwanae.

Chanzo - EATV

Aliyemuua askari ajirusha kutoka kwenye gari ya polisi na kufariki dunia


Mtuhumiwa wa ujambazi aliyefahamika kwa jina Jacob Kideko maarufu kwa jina LA Kichwaa ambaye anadaiwa kumuua Askari mmoja wa Jeshi la Polisi amefariki dunia kwa kujirusha kutoka kwenye gari ya polisi baada ya kukamatwa mjini Morogoro.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoania Arusha Justine Masejo amesema tukio hilo limetokea eneo la Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha wakati mtuhumiwa huyo akirejesha Arusha kutoka Morogoro kwaajili ya kuja kujibu tuhuma za mauaji ya Askari Damas Magoti analodaiwa kulifanya July 23/2021 katika kijiji cha Makiba wilayani Arumeru

Marehemu alifari njiani wakati akiwahishwa katika hospitali ya rufaa ya mount Meru, na mwili wake umehifadhi hospitalini hapo kwaajili ya utambuzi.

USIKIVU WA TBC WAPANDA KWA ASILIMIA 14 NDANI YA MIEZI MIWILI

1 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Innocent Bashungwa(Mb), na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe.Dkt. Faustine Ndungulile (Mb);wakikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Kituo cha kurushia matangazo ya Redio ya TBC eneo la Kisaki - Morogoro leo Julai, 2021.

1Mtaalam wa Mitambo akitoa maelezo kwa  viongozi  mbalimbali waliohudhuria  kwenye ya uzinduzi wa Kituo cha kurushia matangazo ya Redio ya TBC eneo la Kisaki - Morogoro leo Julai, 2021.




Na John Mapepele, WHUSM

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe Innocent Bashungwa amesema hadi kufikia Mwezi Septemba, mwaka huu usikivu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) utapanda kuzifikia Wilaya 120 sawa na 76% kutoka Wilaya 103 ambapo ni sawa na 64% za usikivu wa sasa ili kuhahakikisha wananchi wote wanapata habari kwa uhakika.

Mhe. Bashungwa ameyasema hayo leo Julai 30, 2021 kwenye uzinduzi wa kituo cha kurushia matangazo ya redio eneo la Kisaki mkoani Morogoro ambapo amesema katika Bajeti ya Maendeleo ya Wizara yake kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021, TBC inatekeleza miradi ya upanuzi wa usikivu katika Wilaya za Karagwe (Kagera), Same (Kilimanjaro), Sikonge (Tabora), Kahama (Shinyanga), Bunda (Mara), Nkasi (Rukwa) na Kasulu (Kigoma)ambapo amefafanua kuwa kukamilika kwa miradi hii kutawezesha usikivu wa TBC kufikia 76% ya nchi nzima.


"Nataka kuwahakikishia wananchi wote kuwa Serikali ya awamu ya Sita chini ya Uongozi shupavu wa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakusudia kupanua usikivu wa redio za TBC nchi nzima" amesisitiza Mhe. Bashungwa

Ameyataja maeneo mengine ambayo miradi inaendelea kutekelezwa kwa ushirikiano wa TBC na UCSAF kuwa ni pamoja na wilaya za Ngara (Kagera), Kyela (Mbeya), Ruangwa (Lindi), Kilombero/Mlimba (Morogoro), Ludewa (Njombe), Tanganyika (Katavi), Makete (Njombe), Uvinza (Kigoma), Mbinga (Ruvuma) na Ngorongoro (Arusha).

Pia ametoa wito kwa Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kupeleka miundombinu ya umeme kwa vituo vyote ambavyo vinatumia genereta mfano Karagwe ili kuendelea kupunguza gharama za uendeshaji wa miradi hii.

"Kabla ya mradi kuanza kutekelezwa TBC, TANESCO na UCSAF kaeni pamoja mjadiliane namna ya kutekeleza miradi hii kwa ufanisi ili kutatua shida zinazowakabili wananchi wetu kwa kukosa huduma ya Habari na Mawasiliano" amesisitiza Mhe. Bashungwa

Kwa upande mwingine ameiomba Wizara ya Ujenzi kupitia TANROADS na TAMISEMI kupitia TARURA waone namna ya kuwezesha kufikika eneo hilo la mradi wa Kisaki kwa urahisi zaidi.

"Ombi hili ni sambamba na maeneo mengine yenye mitambo ya kurusha matangazo ambayo miundombinu yake haiko vizuri mfano eneo la Mnyusi- Tanga, Imagi – Dodoma, Matogoro – Songea na Mlima kampuni – Katavi)". Ameongeza Mhe. Bashungwa.

Amesema kuwa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (Ibara 125) inaelekeza Serikali kuhakikisha kuwa inawekeza katika uimarishaji wa miundombinu ya utangazaji kwa TBC.

Mhe. Bashungwa amefafanua kuwa kwa namna ya pekee ibara ya 125 (f) inalekeza kuwa Serikali itahakikisha kuwa "inaimarisha Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kwa kulijengea uwezo wa rasilimaliwatu, fedha na vifaa vya kisasa ili liweze kufikisha matangazo ya redio na televisheni nchini kote kwa ubora na usikivu mzuri....".

Aidha amesema Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka mitano (2020/2021 - 2025/2026) umeainisha vipaumbele vyake katika uwekezaji wa miundombinu ya Utangazaji ya TBC, ikiwemo upanuzi wa usikivu wa redio, pamoja na miundombinu yake.

Ameisihi Menejimenti ya Shirika hilo kuendelea kuwa wabunifu katika kuhabarisha umma na kuwahakikishia kwamba Wizara yake itaendelea kuwapatia msaada wowote wanaohitaji ili kutimiza malengo yake. Amelitaka TBC kuhakikisha linaandaa maudhui yatakayokidhi matakwa ya jamii nzima ya watanzania katika kukuza uzalendo, kudumisha mila na desturi za Watanzania na kulinda tunu za Taifa.

Pia amelipongeza TBC kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuwahabarisha wananchi wa makundi yote, ambapo amesema anatambua jitihada zinazofanywa za kukamilisha uzinduzi wa chaneli mpya ya televisheni ya TBC2 itakuwa mahususi kwa ajili ya vipindi vya vijana, michezo na burudani ambayo ujenzi wa studio zake umekamilika Mikocheni, Dar es Salaam.

Amewashukuru wadau wote ambao wanafanikisha utekelezaji wa mradi wa usikivu wa TBC hapa nchini. Amewataja baadhi ya wadau hao kuwa ni pamoja na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Maendeleo ya jamii,Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa kuendelea kufadhili miradi hii ya Upanuzi wa Usikivu ambayo inatarajiwa kutatua changamoto za Usikivu hivyo kuwezesha wananchi kupata huduma ya habari na Mawasiliano kwa urahisi zaidi.

Amesema uzinduzi wa kituo hiki ni hatua muhimu katika kutekeleza malengo Serikali katika kufisha habari kwa wananchi wote, mahala popote kwa lengo la kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha kwa njia ya redio, televisheni na mitandao ya kijamii. TBC kikiwa ni chombo cha Utangazaji cha Umma, kimetekeleza jukumu hili kwa vitendo.



Matangazo ya Redio za TBC kupitia kituo hiki yanatarajiwa kuwafikia wananchi katika vijiji vya Mvuha, Dhutumi, Bwakila Chini, Dakawa, Mngazi, Milengwelengwe, Sesenga, Nyalutanga, Mdokonyole, Gomelo, Kisaki Station, Matambwe, Kolelo, Lukange, Mgata, Ngerengere, Singisa na kwingineko). Maeneo mengine yatakayonufaika na mradi huu ni katika Wilaya za jirani za Kilombero, Rufiji na Kilwa.

"Kuzinduliwa kwa matangazo ya Redio katika kituo hiki cha Kisaki, ni utekelezaji wa Ilani ya CCM (2021 – 2025), ikiwa ni mwaka mmoja tu tangu kuzinduliwa kwake".amesisitiza Mhe. Bashungwa.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...